Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kesi ya Trump: Nambari nne zinazoelezea kwa nini rais Trump hakupatikana na hatia
Baada ya kesi iliyochukua takribani wiki mbili rais wa Marekani Donald Trump ameondolewa mashtaka na sasa anaweza kuendelea kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao.
Ni matokeo yaliotarajiwa, lakini njia iliotumiwa kufikia uamuzi huo ndio iliyovutia.
Hizi hapa ni nambari nne zinazoelezea kesi hiyo. Na kile kitakachofanyika sasa.
Kuondolewa kesi kwa bwana Trump katika bunge la seneti kunaonesha umaarufu wake miongoni mwa wanachama wa chama cha Republican.
Iwapo haikuwa wazi kabla ya kesi hiyo kwamba alikuwa na uungwaji mkono katika wadhfa wake na chama chake basi ni wazi hivi sasa.
Hajawahi kupoteza umaarufu miongoni mwa wanachama wa Republican ama hata kuongeza umaarufu miongoni mwa wanachama wa Democrats.
Kulingana na kura ya maoni iliofanywa na Gallup wiki hii asilimia 94 ya Republicans wanaunga mkono utendakazi wa bwana Trump tangu achukue mamlaka.
Takwimu hizi zimeendelea kuimarika licha ya kesi iliokuwa ikimkabili.
Gallup pia iliripoti kwamba asilimia 89 ya wanachama wa Republican walimuunga mkono rais Trump katika mwaka wake wa tatu uongozini - hii ilimfanya kuwa rais wa pili mwenye umaarufu mkubwa kwa wakati wake kama rais miongoni mwa wanachama wa chama chake.
Haikuwa hivi. Miaka minne iliyopita wakati ambapo maafisa wakuu wa chama cha Republican walikuwa wanajiandaa kumshutumu rais Trump, mtu ambaye hatimaye alikuwa chaguo la chama chake kuwania kitu cha urais.
Mwaka 2016, seneta wa jimbo la Alaska, Lisa Murkowksi aliapa kutompigia kura . ''Iwapo tutamchagua Trump tutaharibikiwa'', alisema seneta wa jimbo la Carolina kusini Lindsey Graham.
Bwana Trump aliteuliwa kuwakilisha chama cha Republican na maseneta wote wawili bi Murkowski na Graham walikuwa katika sakafu ya bunge la seneti wakati wa kesi yake ili kumuunga mkono.
Kama ilivyodhihirishwa wakati wa uchaguzi wa kati kati wa 2018, wakati ambapo wanachama kadhaa wa chama cha Republican ambao hawakumuunga mkono bwana Trump walipoteza viti vyao , ambapo wafuasi wa chama cha Republican walikataa kumsamehe yeyote ambaye hakumuunga mkono rais Trump.
Umaarufu wake hata hivyo haumaanishi kwamba wafuasi wake wanaamini kwamba hakuwa na makosa katika kesi hiyo.
Katika kura ya maoni iliofanywa na AP na sio kituo cha utafiti wa umma NORC, wiki iliyopita asilimia 54 pekee ya wanachama wa Republicans wanaamini hakufanya makosa.
Wanachama wa Repiublican katika bunge la seneti wana wingi wa viti 53 dhidi ya 47 vya Democrat, ikimaanisha kwamba waliweza kutawala bunge hilo na kwamba waliweka masharti ya kesi hiyo.
Wingi huo ulikuwa muhimu. Wakati wa kesi, maseneta walilazimika kupiga kura kuhusu iwapo wangeweza kuleta mashahidi na wengi wao wakakataa.
Iwapo wanachama wanne wa Republican wangepiga kura upande mwengine , mashahidi wangeruhusiwa hususan aliyekuwa mshauri wa baraza la usalama John Bolton ambaye ushahidi wake ungekandamiza kesi hiyo ya Trump.
Wabunge wanne wa Republican waliyumba, seneta wa jimbo la Utah, Mitt Romney miongoni mwao.
Wakati mmoja walionekana kana kwamba watapigia kura upande wa Democrat na maseneta huru na kuruhusu kuleta mashahidi, lakini mwishowe, wanachama wote wa Republican walipiga kura kuunga mkono chama chao, na hakuna mashahidi walioletwa, hatua iliyokamilika baada ya siku 15 pekee.
Hii ndio nambari iliohakikisha kuwa Trump angeondolewa mashtaka. Angepatikana na hatia iwapo asilimia mbili ya maseneta 67 wangeunga mkono.
Hii ingehitaji maseneta 20 wa Republican kumpigia kura rais wao ili kumpata na hatia. Mwisho ni seneta mmoja pekee aliyefanya hivyo, Mitt Romney.
Hiki ndicho kiwango cha fedha ambacho kampeni ya rais Trump inasema kwamba ilichangisha katika robo ya mwisho ya mwaka 2019, ikiwa asilimia kubwa ya wafuasi wa Trump wakijibu hatua ya kushtakiwa kwake.
Umaarufu wa rais Trump mashinani unaweza kumfanya achaguliwe tena, alisema meneja wake wa kampeni Brad Parscale.
Baada ya kesi hiyo kupita , rais Trump sasa yuko huru kuendelea na kampeni zake za uchaguzi ujao ijapokuwa ukweli ni kwamba hakuruhusu kesi hiyo kuzuia kampeni yake.