Donald Trump: Miaka ya kuharibika kwa uchumi imekwisha
Rais wa Marekani Donald Trump amesifu kile alichokiita ''kurejea tena kwa Marekani '' kwenye hotuba aliyoitoa kwa bunge la congress wakati huu wa mchakato wa kumuondoa madarakani ukitarajiwa kushindwa.
Akitoa hotuba yake ya mwaka , Trump ameeleza matumaini yake ya kuimarisha uchumi wa Marekani akiwa na matumaini ya kuwa na miaka mingine minne madarakani
''Miaka ya kuharibika kwa uchumi imekwisha,'' alieleza.
Trump wakati wote alikwepa kuzungumzia moja kwa moja kuhusu wabunge waliojaribu kumuondoa madarakani.
Wabunge wa Republican waliimba ''miaka minne tena'' wakati Trump alipokuwa anajiandaa kuzungumza.

Chanzo cha picha, MANDEL NGAN/AFP via Getty Images
Namna ambavyo Trump alikutana Pelosi
Kabla ya Bw. Trump kuanza kuzungumza kwenye membari ndani ya bunge, alikataa kumpa mkono Spika Nancy Pelosi.
Bibi Pelosi, wakosoaji waligundua, aliruka utaratibu wa kawaida wa kumpokea rais kwa heshima kama utangulizi.
Ilikuwa ni mara ya kwanza Bwana Trump kukutana uso kwa uso na adui yake wa kisiasa tangu atoke kwenye mkutano wa White House miezi nne iliyopita.
Wakati rais alishtumu Democrat kwa kupanga kuwalazimisha walipa kodi wa Marekani kutoa huduma ya afya ya bure kwa wahamiaji wasio na nyaraka , Bi Pelosi alionekana mara mbili akisema: "Sio kweli."
Bi Pelosi alinyanyuka zaidi ya mara moja kumpongeza rais , ikiwemo wakati alipokuwa akinadi mradi wa uwekezaji wa miundombinu.
Rais amesema nini zaidi?
Akikemea japo si moja kwa moja kuhusu sera za mtangulizi wake Barack Obama, Trump alisema: ''Katika kipindi kifupi cha miaka mitatu, tumezima mawazo kuhusu kuanguka kwa Marekani na tumekataa kuupunguza mustakabali wa Marekani.
''Tunasonga mbele kwa kasi ambayo haijawahi kufikiriwa muda mfuoi tu uliopita, na haturudi nyuma!''
Mara kwa mara alitupa lawama kwa Democrats, ikiwemo wagombea wa mrengo wa kushoto kama vile Bernie Sanders ambao wanapambana kumuondoa madarakani
''Hatuwezi kuruhusu ujamaa uharibu sekta ya afya ya Marekani! alisema rais, ambaye wakosoaji wake wameeleza kuwa pamoja na kupinga hajawahi kuja ni mipango yake mwenyewe kuhusu masuala ya afya.

Chanzo cha picha, AFP
Wageni walikuwa nani?
Rais alialika wageni kadhaa maalumu, akiwemo kiongozi wa upinzaji wa Venezuela, Juan Guaido, Wanajeshi wa zamani wawili na kaka wa mtu aliyeuliwa na mhamiaji asiye na nyaraka.
Katika harakati fulani za kuchochea wakosoaji wake, Bwana Trump alitangaza kuwa atatoa tuzo ya heshima ya juu kabisa ya raia wa Marekani, kwa mtangazaji wa redio ya kihafidhina Rush Limbaugh, ambaye aliweka wazi kuwa na saratani ya mapafu.
Mwanzoni Lady Melania Trump alitoa heshima hiyo kwa mhemko Limbaugh wakati rais alizungumza.
Mtu mmoja alisindikizwa akitolewa wakati Bwana Trump alipokuwa akitetea haki za kumiliki bunduki. Iliripotiwa kuwa Fred Guttenberg ni baba ya Jaime Guttenberg, mwanafunzi aliyeuawa katika shambulio la shule huko Parkland, Florida, mwezi Februari 2018.
Bwana Guttenberg alikuwa mgeni wa Bi Pelosi.
Democrats wamesema nini?
Kama walivyofanya mwaka jana, Wafuasi wengi wa kike wa Democrat pamoja na Bibi Pelosi - walivaa mavazi meupe kuwakumbuka wapigania haki ya wanawake wa Marekani kupiga kura mwaka 1920.
Wabunge kadhaa wa Democrat akiwemo Alexandria Ocasio-Cortez wa New York na Maxine Waters wa California, walisusia hotuba ya Trump.
Bi Ocasio-Cortez alitoa maoni kwamba "sitatumia uwepo wangu katika hafla ya serikali kusafisha hali ya ukiukaji wa sheria na Katiba".
Gavana wa Michigan kutoka chama cha Democrat Gretchen Whitmer. alimshtumu rais kwa kushindwa kurekebisha shida za Amerika. "Kuwadhalilisha watu kwenye mtandao wa Twitter hakuwezi kurekebisha madaraja-kunazidi kuyaharibu,'' alisema. wa kudhulumu kwenye mtandao wa Twitter hawarekebishi daraja - inawachoma," alisema.














