Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mexico yawazuia wahamiaji kuingia Marekani
Mamia ya wahamiaji ambao waliingia kupitia mto katika eneo la mpaka wa kusini mwa Mexico wamezuiwa kuingia nchini humo walipokua njiani kuelekea Marekani .
Wahamiaji hao ambao wengi wao wanatoka katika taifa la Honduras waliamua kutumia njia ya maji baada ya kupata ruhusa yaya kuvuka kupitia daraja lililopo karibu.
Vikosi vya usalama vilifyatulia vitoa machozi kuwalazimisha wahamiaji na kurudi nyuma kuwazingira wale ambao waliweza kuvuka mpaka.
Mexico imefunga njia za wahamiaji zinazoelekea nchini Marekani kutokana na shinikizo la rais Donald Trump.
Vikosi vya National Guard vilivyokua vimebeba ngao za kujikinga na mashambulizi ya ghasia vilionekana vikijaribu kuwazuia wahamiaji kupanda kingo za mto Suchiate, ambao ndio mpaka baina ya Mexico na Guatemala.
Baadhi ya wale ambao walijaribu kufika Mexico waliwarushia mawe polisi.
Wahamiaji waliokamatwa wamehamishiwa katika vituo vya uhamamiaji. Watarejea katika nchi zao kama uhamiaji waokisheria hautatuliwa, serikali imesema.
Wahamiaji wamekuwa wakikita kambi nje nchini Guatemala katika mji wa Tecun Uman, kwenye mpaka na Mexico wa Ciudad Hidalgo.
Wawakilishi wanane wa wahamiaji waliruhusiwa kuingia Mexico kwa mazungumzo na mamlaka na kufikisha barua yao kwa rais Andrés Manuel López Obrador.
Walimuomba awaruhusu wapite na wakaahidi kuheshimu sheria.
Wale waliojaribu kuvuka mpaka Jumatatu walikua ni sehemu ya kikundi cha wahahamiaji kati ya 2,000 na 3,500-lililopewa jina la "2020 Caravan", azma yao ya kuvuka Mexico kwa wingi ili kuingia Marekani ilikataliwa.
Kwa upande wake,Guatemala ilisema maelfu kadhaa ya wahamiaji wamevuka mipaka yake na kuingia nchini humo kutoka Honduras tangu Jumatano.
Wengi wa wahamiaji katika mpaka wa Mexico walisema kuwa wanakimbia ghasia, umaskini na viwango vya hali ya juu vya mauaji.
"Tumetaka sana kuondoka kwasababu joto limetuchosha sana hususani kwa watoto," Mhamiaji wa Hondurus grant Elvis Martinez aliliambia shirika la habari la AFP.
Mexico imesema kuwa wanaweza kuishi na kufanya kazi nchini Mexico na kutuma maombi ya uhamiaji, lakini hawataruhusiwa kupata njia ya kuelekea Marekani.
Unaweza pia kusoma:
"Wanajaribu kutulaghai. Wanatuambia tujisajili, lakini wanaturejesha tulikotoka ," alisema mhamiaji mwingine.
Waziri wa mambo ya ndani wa Mexico alisema kuwa tayari wamekwisha wachukua wahamiaji 1,100 katika majimbo ya Chiapas Tabasco. Wengi miongoni mwao watarejeshwa katika nchi zao za asili ''kama hali zao zitawaruhusu "
Rais wa Marekani Donald Trump alisaini makubaliano na Mexico mwezi Juni ya kuwazuia wahamiaji kuingia Marekani baada ya kuongeza ushuru wa bidhaa zake. Mexico ilichukua hatua ''za dharura'' za kukabiliana na uhamiaji mkiwemo kuwapeleka askari wake National Guard katika maeneo ya nchi yanayotumiwa na wahamiaji kuingia Marekani.
Makubaliano mengine na Guatemala, yalikua ni kwamba ni ''chi ya tatu salama ". Chini ya mkataba, Marekani inaweza kuwatuma wahamiaji kutoka Honduras au El Salvador waliopitia Guatemala kurudi katika nchi hiyo kuomba uhamiaji kwanza.
Bwana Trump ameyafanya mapambano dhidi ya wahamiaji haramu kuwa sera kuu ya Marekani na amechukua hatua kuwazuia kuingia nchini Marekani kwa kupitia mpaka wa Mexico, ikiwemo mipango ya ujenzi wa ukuta wa mpaka.