GHB: Dawa hii inatumika kama 'silaha ya hiari ya ubakaji'

Iliyochapishwa

Wakati Reynhard Sinaga alipomrejesha mwathirika nyumbani kwake, angewatilia dawa hiyo kabla ya kuwanyanyasa kingono.

Baada ya kupatikana na hatia kwa makosa 159 ya kingono, waziri wa mambo ya ndani Priti Patel aliagiza kupitiwa tena kwa sheria ya udhibiti wa dawa kama GHB.

Dawa ya GHB ni nini?

Japo wakati mwingine inafahamika kama dawa inayompoteza mtu fahamu na kumfanya kuwa katika hatari ya kushambuliwa kingono, dawa ya GHB inatumika kwa kujiburudisha.

Mara nyingi hutumika na wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wakati dawa inatumika kuongeza ashki kati ya wapenzi wawili au zaidi lakini pia inatumika na wapenzi wa jinsia tofauti kama dawa ya kunogesha mapenzi.

Lakini wabakaji wanaotumia dawa ya GHB kwa ajili ya kuongeza ashki - utafiti wa hivi karibuni unaashiria kwamba zaidi ya robo ya watu wanaoitumia, walivamiwa kingono wakiwa hawana fahamu ya kile kinachoendelea.

GHB ni dawa tofauti lakini inafanana kwa karibu sana na dawa ya kimiminika ya GBL (gamma-butyrolactone), inayoruhusiwa kisheria lakini inabadilika na kuwa dawa ya GHB ikishaingia mwilini.

Kw apamoja zinafahamika kama "G", na zote ni angavu, zisizo na harufu na za majimaji na zenye mafuta ambazo huchanganywa kwenye vinywaji.

Dawa hii inafanya nini?

Dawa hii inaweza kumfanya mtumiaji kupata msisimuko na kuongeza hashiki au hamu ya ufanya tendo la ngono lakini kunywa zaidi ya kipimo stahiki hata kwa chini tu ya mililita kunaweza kusababisha kifo.

Kutumia kiwango cha juu cha dawa, jambo ambalo ni rahisi sana kutokea hasa inapochanganywa na pombe au dawa nyengine, na pia nguvu ya dawa ambayo hubadilika kulingana na chupa - inaweza kufanya mtumiaji kwa kuanza kupayuka, mwili kuanza kukakamaa kama mwenye kifafa, kupoteza fahamu na kuaha kupumua.

Professor Adam Winstock, mshauri wa magonjwa ya kiakili na mwanzilishi wa utafiti wa dawa ulimwenguni: "Ni dawa ambayo ni hatari sana kwa watu wanaoitumia kama kuburudisho."

"Ikiitumia tone moja zaidi ya inavyohitajikaya dawa ya GHB, dakika 20 baadaye unapoteza fahamu," anasema.

Ni vifo vingapi vilivyohusishwa na dawa ya GHB?

Kulingana na takwimu rasmi kutoka Shirika la takwimu za kitaifa, vifo 120 Uingereza na Wales vilitokana na dawa hiyo kati ya mwaka 2014 na 2018.

Lakini idadi kamili huenda ikawa juu zaidi kwa sababu si kawaida watu kufanyiwa vipimo vya sumu wanapokupa ghafla. Kulingana na Profesa Winstock, dawa hiyo ni vigumu kupatikana na pia ghali mno.

Na je mashambulizi ya kingono?

Ni vigumu sana kufahamu ni idadi kamili ya watu walioshambuliwa kingono baada ya kutumia dawa ya GHB.

Kabla ya Sinaga kupatikana na hatia, pengine mtu wa ngazi ya juu zaidi kupatkana na hatia alikuwa ni muuaji Stephen Port, aliyehukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2016 kwa makosa ya mauaji ya vijana wanne kwa kuwatilia sumu ya lethal.

Kati ya wapenzi 2,700 wa jinsia moja na wale wanaoshiriki mapenzi na watu wa jinsia zote ambao wamewahi kutumia dawa ya G walioshiriki utafiti uliofanywa na BuzzFeed News na kipindi cha Dispatches cha Channel 4 uliofanywa mwaka jana, asilimia 28 walisema wamewahi kushambuliwa kingono.

Mhariri wa masuala ya watu wa jinsia moja wa BuzzFeed News' Patrick Strudwick, na mtangazaji wa kipindi cha masuala ya ngono, dawa za kulenya na mauaji cha Channel 4, waliitaja dawa hii kama "silaha ya hiari ya ubakaji mwaka 2020".

"Kwasababu inaweza kuingizwa kwenye kinywaji cha mtu bila yeye mwenye kufahamu, na pia kwasababu inamfanya mtu kupoteza fahamu haraka sana, hii ni dawa ambayo inatumiwa kwa urahisi na wavamizi," amesema.

kikwazo kikubwa katika kufahamu ukubwa wa tatizo ni kwamba mara nyingi waathirika hawaripoti tatizo hili kwa polisi, amesema profesa Winstock.

Mtu anaweza asifahamu kile kilichotokea na iwapo kuna uhalifu uliotendeka, amesema, pia anaweza akahisi kuabika, kuhukumika na kupata hofu "ya kuzungumza kwa uwazi kile alichopitia ambacho huenda kikawa aibu", amesema.

Wengi pia wanahofia kwamba huenda wakachunguzwa kwa madai ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Je dawa hii inaweza kumfanya mtu akawa mraibu?

Bila shaka, hili ni jambo ambalo linaweza kutokea kwa haraka mno na Profesa Winstock anaonya kwamba mtu yeyote anayekunywa dawa hii kila siku haruhusiwi kuacha kuitumia bila msaada wa daktari.

"mtu anaweza kuwa mtegemezi na kuacha kuitumia kunaweza kuhatarisha maisha," anasema.

Madhara ya muda mrefu ya kutumia dawa hii bado hayajafahamika.

Upatikanaji wake uko vipi?

Kama dawa nyingine nyingi haramu, upatikanaji wa dawa hii ni vigumu sana kubainika kwasababu haipo katika utafiti wa matumizi ya dawa unaofanywa kitaifa.

Lakini Strudwick amesema dawa ya G " ni rahisi sana kupatikana na kuinunua iwapo unaufahamu wa kule inapopatikana na kwasababu ya mianya ya kisheria, hii inamaanisha kwamba dawa ya GBL inaweza kuuzwa kwa matumizi ya viwandani mfano kwa ajili ya kuondolea rangi na matumizi mengineo.

"Uingereza, makampuni wanaiuzia watu baada ya kuitangaza mitandaoni... na ikishauzwa kwa wingi, inaweza kusambazwa kwa wanunuzi wengine wanaohitaji kwa kiasi kidogo kupitia mitandao ya wanaopendana kama ule wa Grindr," amesema.

Chimbuko la dawa ya GHB?

GHB ilibuniwa miaka ya 1960 kama dawa ya ganzi lakini ikapigwa marufuku kwa sababu ya madhara yake.

Miaka ya 1980, ilitumika kama dawa inayosaidia mtu kupata usingizi na pia njia mbadala ya kujenga mwili.

Je dawa hii ni haramu?

GHB imekuwa katika daraja C tangu mwaka 2003, baada ya kuwekwa chini ya kifungu cha matumizi mabaya wa dawa.

Hata hivyo dawa ya GBL ni halali kutumika viwandani, pia nayo imewekwa katika daraja C tangu mwaka 2009 na yeyote anayeisambaza ama kuwa nayo akiwa na nia kwamba itatumika, ni uvunjaji wa sheria.

Kuwa na dawa zote hizo kuna weza kusababisha kifungo cha miaka miwili gerezani ama pia unaweza kupigwa faini kulingana na jaji husika, na kusambaza dawa hizo kuna weza kusababisha kifungo cha miaka 14 ama au bila hata ya faini.

Profesa Winstock anasema kuongeza vitengo hakutaleta tofauti yoyote na kwamba kutafanya watu wasite kutafute usaidizi.

Badala yake anasema serikali inastahili kuangazia zaidi kuelimisha watu kwamba dawa hizo zinaweza kutumika kwa njia salama zaidi pamoja na kuhamasisha majadiliano ya wazi kuhusu vile wanavyozitumia.

Familia ya Eric Michels, aliyekufa baada ya kunywa kiwango cha juu cha dawa ya GHB mwaka 2018, imekuwa ikifanya kampeni ya dawa hiyo kujumuishwa katika daraja la A la dawa.

Kijana wake Sam ameiambaia BBC kwamba ni dawa mbaya sana ambayo imeua watu wengi akiwemo baba yake.