Je, hati ya kusafiria ya Malta ina manufaa gani?

Ujumbe wa Muungano wa Ulaya utazuru Malta kuchunguza sheria inayotumika huku kukiwa na athari kuhusu uchunguzi wa mauaji ya mwandishi mmoja.
Mauaji ya Daphne Caruana mwaka 2017 yamewayumbisha wanasiasa na kuangazia hofu kubwa kuhusu madai ya ufisadi na idara ya mahakama iliyo hafifu katika kisiwa hicho cha Mediterean.
Biashara ya 'pasipoti za dhahabu' kama inavyoitwa imekuwa ikishamiri miongoni mwa watu matajiri wanaotafuta eneo lililo na kodi ya chini, wasomi ama hata taifa jipya ili kuanza makao kutokana na sababu zao za kisiasa.
Lakini je uraia unaweza kukugharimu kiwango gani cha fedha katika kisiwa cha Malta na ni nini haswa tunachokijua kuhusu watu wanaonunua hati za kusafiria za Malta?.
If you bring €900,000, you can buy a Maltese passport and then you become an EU citizen."
Jinsi unavyoweza kununua uraia Malta

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Malta ilizindua mpango huo mwaka 2014 ili kuwavutia watu matajiri na uwekezaji. Ili kujipatia pasipoti , wanaotuma maombi watahitajika kutekeleza yafuatayo:
- Kuchagngia €650,000 (£554,000) katika hazina ya kitaifa ya maendeleo
- Kuweka €150,000 katika soko la hisa la Malta
- Kununua mali isiopungua €350,000 (ama kukodi moja ya gharama ya €16,000 kwa mwaka )
Kwa jumla hiyo ni €1,150,000, zikiwa ni zaidi ya gharama ya €900,000 inayotolewa na mwanasiasa wa Uholanzi Sophie.
Wanaotuma maombi ni sharti pia wawe wameishi katika kisiwa hicho kwa zaidi ya miezi 12, ijapokuwa sio lazima wawe wameishi nchini humo kimwili.
Kumekuwa na wawekezaji 833 na familia 2,109 ambazo zimepata uraia wa Malta tangu mpango huo uanzishwe.
Pasipoti ya Malta inawaruhusu wamiliki wake kuwa na viza ya kusafiri katika mataifa mengine kwa kuwa Malta ni mojawapo ya mataifa yanayotumia Visa yenye makubaliano ya Schengen.
Katika katikati ya mwaka 2017 na katikati ya 2018, mpango huo ulikusanya €162,375,000 sawa na asilimia 1.38% ya mapato ya uchumi wa Malta katika kipindi hicho, ijapokuwa mwaka 2018 idadi ya watu wanaotaka kununua uraia ilipungua.
Kuna motisha kwa mataifa madogo kama Malta kuwa na mipango kama hii ili kuvutia kiwango kikubwa cha uwekezaji.
Mataifa mengi madogo yamekuwa yakitegemea mapato yanayotokana na mipango kama hiyo, kulingana na Luuk van der Baaren, mtafiti wa uhamiaji katika taasisi ya chuo kikuu cha Ulaya mjni Florence.
Je ni akina nani wanaonunua pasipoti ya Malta?
Serikali ya Malta haitoi habari kuhusu wanakotoka matajiri hao lakini hutoa habari za eneo wanalotoka.
Wengi wanaotuma maombi hutoka Ulaya wakifuatiwa na raia kutoka eneo la mashariki ya kati , eneo la Ghuba na Asia.
Hata hivyo wanachama wa mataifa ya Ulaya wanaruhusiwa kuchapisha takwimu kuhusu uraia mpya mwaka huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya uzinduzi wa sera hiyo nchini Malta 2014 kulikuwa na ongezeko la idadi ya watu waliopata uraia kutoka Saudi Arabia , Urusi na China. Kwa mfano Saudia haikuchangia idadi ya raia wanaotafuta uraia kabla ya 2015 lakini tangu wakati huo kumekuwa na zaidi ya watu 400 kutoka taifa hilo.
Kuna sababu muafaka za kutafuta uraia mwingine lakini kuna madai kwamba mpango huo wa Malta unatumiwa vibaya.
Tume ya bara Ulaya ilichapisha ripoti yake mwezi Januari 2019 ikisema kwamba ina malalamishi kuhusu mpango huo wa malta ambao hauna masharti mengine ukilinganishwa na mataifa mengine la Muungano wa Ulaya.
Kwa mfano , wanaotuma maombi hawalazimishwi kuwa na anwani ya kuwepo nchini humo na hakuna masharti ya kuwa na mipango yoyote katika taifa hilo.
Serikali ya Malta inasema kwamba huwachunguza wote wanaotuma maombi pamoja na wanasiasa maarufu.
Bwana Van der Baaren anasema kwamba familia nyingi huweza kutumia taifa hilo ili kuwasomesha wanao ughaibuni ama kumiliki pasipoti hizo iwapo wanataka kuondoka kutoka taifa lao, lakini anaongeza: Mipango hiyo pia inaweza kuzua swala la usawa kutoka katika mataifa wanayotoka watumaji maombi kwa kuwa unaruhusu watu wachache walio matajiri kununua uraia wa pili.
Katika muungano wa Ulaya Cyprus na Bulgaria zina mipango kama hiyo. Kati ya mwaka 2008 na 2018, Cyprus iliwapatia uraia wake wawekezaji 1,685 na watu 1,651 wa familia .
Ijapokuwa mwezi Novemba , taifa hilo liliwapokonya wawekezaji 26 pasipoti za taifa hilo kutokana na makosa yaliofanyika wakati wa kutengeza vibali hivyo.













