Waliopata elimu ya juu kwa mkopo nchini Kenya mashakani

Pesa ya kenya

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Ikiwa wewe ni mmojawapo wa Wakenya 85,000 ambao bodi ya elimi ua juu nchini Kenya inasema hawajalipa mkopo wa elimu ya juu huenda ukawa mashakani.

Bodi hiyo kwa kifupi helb inasema itawataja majina na kuwaabisha watu wote ambao hawajalipo mikopo yao ya gharama ya masomo ya chuo kikuu katika kipindi cha siku 30.

Helb, ambayo imekuwa imekuwa ikiwasaka watu waliosoma kwa mkopo kila kona, inasema kuwa itachapisha picha za wanaume na wanawake wenye madeni ambao wameshindwa kulipa madeni yao, ambayo kwa sasa yamefikia shilingi bilioni 50 za za Kenya.

Katika taarifa yake iliyoitoa Jumapili na kushirikishwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya Wakenya, bodi hiyo imesema wenye deni hilo watatakiwa kujiytokeza na kueleza ni vipi watalipa mikopo yao:

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Tangazo hili la Helb limeibua hisia mbali mbali katika mitandao ya kijamii nchini Kenya, huku watumiaji hususan wa mtandao wa twitte, huku baadhi wakishauri serikali kutatua matatizo yake badala ya kuwaaibisha waliochukua mikopo ya masomo wasio na ajira:

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Baadhi walitumia picha za wanyama kuonyesha mshangao wa Wakenya kufuatia tangazo la Helb:

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Bodi hiyo inayodhamini elimu ya juu nchini Kenya inasema kuwa inahitaji fedha hizo ili kuwasaida Wakenya wengine maskini kufikia ndoto zao za kupata Shahada na Stashahada.

Helb inasema kuwa baadhi ya watu walionufaika na mkopo ambao bado wanadeni walishindwa kujibu mawasiliano ya awali na hivyo kukwamisha utoaji wa msaada wa fedha kwa Wakenya wengine wanaostahili.

" Majina na picha za watu wenye deni la Helb ambao hawajalipa deni lao tangu mwaka 1975 hadi leo yatachapishwa katika magazeti makubwa nchini Kenya baada ya siku 30 kuanzia siku lilipotolewa tangazo na baada ya hapo hatua a kisheria zinawea kuchukuliwa dhidi ya kila mtu mwenye deni ," liliongeza tangazo hilo.

Bodi hiyo kwa sasa imewataka walionufaika na mpango huo ambao hawalipi mikopo kuwasiliana nayo ili wapewe akaunti ya mkopo.

Unaweza pia kusoma:

Mwaka jana Helb iliweza kupata zaidi ya shilingi milioni 500 kufuatia miaka miwili ya msamaha uliotolewa na serikali.

Kwa mujibu wa Helb, haiwezi kuwapata watu 17,000 wenye deni, huku mwaka jana watu 85,000 walikuwa na deni la bodi hiyo.

Jumla ya wahitimu 169,909 walikuwa wamekamilisha malipo ya mikopo yao yenye thamani ya shilingi bilioni 13.2 kufikia 2017, huku wengine wapatao 136,783 wakiendelea kulipa mikopo yao. beneficiaries were servicing loans worth Sh20.7 billion.

Tangu mwaka 1974, mpango wa utoaji mkopo wa masomo ya elimu ya juu umewasaidia zaidi ya Wakenya 645,000 kupata elimu ya juu kwa thamani ya shilingi bilioni 72 kwa ujumla.