Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Lady Gaga aanguka kutoka jukwaani baada ya kurukia mikono ya shabiki
Lady Gaga aliangukia mashabiki wakati wa onyesho la Muziki Las Vegas.
Nyota huyo alimuita shabiki wake kwa jina Jack kujumuika naye jukwaani na kumrukia mikononi mwake- Lakini Jack hakuwa imara na wawili hao walianguka chini.
''Tulifikiri ameaga dunia,'' aliandika shabiki mmoja mtandaoni.
Badala yake, Gaga alirejea na kutumbuiza kibao chake kiitwacho Million Reasons akiwa sambamba na Jack. ''inashangaza'', ''tunapendana sana tukaanguka jukwaani pamoja.''
''Tulirukiana mikononi . Tulikuwa kama Jack na Rose wa Titanic''.
''Nafikiri tunapaswa kupata kikombe cha chai pamoja.''
Mashabiki walikuwa wakifuatilia hali ya Gaga kwa kuwa ana matatizo ya baridi yabisi hali inayomsababishia maumivu makali.
Mwaka 2013, aliahirisha onyesho lake la Born This Way baada ya kuteguka nyonga.
Lakini muimbaji huyo aliwapa moyo mashabiki wakati walinzi walipomsaidia kunyanyuka.
''Kila kitu kiko sawa,'' alisema. ''kitu pekee ambacho hakiko sawa ni kuwa tunahitaji ngazi ili niweze kupanda.
Pia Nyota huyo alimpa moyo Jack, ambaye alikuwa akilia baada ya tukio hilo.
''Usiwe na wasiwasi, kila kitu kiko sawa. si makosa yako,'' aliongeza: ''Unaweza kuniahidi kitu? unaweza kuacha kujilaumu kwa kile kilichotokea?''
''Alimpandisha jukwaani na kuwasihi kila mmoja mtandaoni kutomkosoa.
Baadae kwenye onyesho hilo, Gaga alithibitisha kuwa ajali hiyo haijasababisha madhara yoyote, alipotumbuiza kibao chake, Bad Romance.