Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa picha: Jamii ya Waoromo ilivyosherehekea tamasha la kutoa shukurani
Maelfu ya watu walijitokeza kusherehekea tamasha la kutoa shukurani maarufu Irreecha lililoandaliwa mjini Addis Ababa kwa mara ya kwanza, na jamii ya Waoromo ambayo ni kubwa zaidi, nchini Ethiopia
Moja ya tamaduni ya Irreecha ni kukata, kukata nyasi na maua na kuweka ndani ya maji kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa kumaliza salama msimu wa mvua na kukaribisha msimu wa masika.
Kulikua na ulinzi mkali huku maelfu ya watu wakijitokeza katika barabara za mji mkuu, na maeneo ya umma mjini Addis Ababa kama vile, ukumbi wa Meskel.
Wengi wao walikua wakiimba na kupeperusha bendera na maua.
Maafisa wa jiji hilo walisema wanatarajia watu milioni 10 kuhudhuria tamasha hilo lakini ni vigumu kukadiria niwatu wangapi waliohudhuria.
Miaka iliopita tamasha hilo liliandaliwa mjini Bishoftu, kilo mita 40 nje ya mji kuu wa Addis, lakini matamasha mengine yalifanywa katika miji tofauti ya jimbo la Oromia, nyakati tofauti za mwaka.
Hatua ya kuandaliwa kwa tamasha la mwaka huu katika mji mkuu wa Ethiopia unaozungukwa na jimbo la Oromia, inachukuliwa kama ishara ya mamlaka nchini kutambua utamaduni wa jamii ya Waoromo. ambayo kwa miaka kadhaa imekua ikidai kutengwa kijamii na kisiasa.
Lakini baadhi ya wadadisi wameiambia BBCkuwa hatua hiyo ni jaribio la chama tawala kupata uungwaji mkono wa jamii hiyo inapojiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Inasadikiwa kwamba kuna jumla ya Waoromo milioni 40 nchini Ethiopia, ambao wanachangia 30% ya idadi ya watu wa nchi hiyo.
Katika jamii hiyo kuna mila tofauti inayohusishwa na mahali mtu alikotoka lakini Irreecha inawaleta pamoja.
Sherehe hiyo inatoa fursa kwa watu kuvalia nguo zao za kitamaduni.
Mwanamume huyu kutoka eneo la Shoa , aamevalia mavazi yanayojulikana kama "Daabe", ambayo hutengenezwa kutokana na ngozi ya nyani.
Shanga zilizovaliwa usoni na wanawake hawa zinaitwa chelie, na huvaliwa na Waoromo wote, lakini nguo zao ni za watu waeneo la Borena.
Wanaume hawa walitembea mwendo wa kilomita 400 kutoka Bale, kusini mwa Ethiopia, kuhudhuria tamasha la mwaka huu. Vitambaa walivyofunga kichwani vinaitwa ruufa, na huvaliwa wakati wa sherehe kubwaare.
Mwanamke huyo kutoka eneo la Hararghe, mashariki mwa Ethiopia, alivalia ngua ya kitamaduni ya eneo hilo.
Jamii ya Alaba, kutoka eneo la kusini mwa Ethiopia ambalo lipo nje ya jimbo laOromia, pia ilihudhuria sherehe hiyo.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Dkt Abiy Ahmed anatokea jimbo la Oromia.
Amefanya mabadiliko makubwa nchini humo tangu alipoingia madarakani mwaka jana kufuatia maandamano ya kushinikiza kutambuliwa kwa haki za jamii tofauti.
Hatua ya Licha kuandaliwa kwa ya tamasha hilo katika jiji Kuu la Addis Ababa inajiri wakati ambapo joto la kisiasa linaripotiwa kupanda huku uhasama wa kikabila ukiendelea kukabili utawala wa Bw. Abiy.
Picha za Yadeta Berhanu (BBC), Amensisa Negera (BBC), Reuters na AFP.