Binti aliyepambana dhidi ya baba yake vitani nchini Ethiopia

Familia ya Alemtsehay Kasa

Chanzo cha picha, Alemtsehay Kasa

Iliyochapishwa

Kamanda wa polisi nchini Ethiopia ameisimulia BBC jinsi binti yake alipojiunga na kundi la waasi akiwa mdogo- binti yake alijiunga na kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF) mwishoni mwa miaka ya 1970 na kupigana na baba yake katika uwanja wa vita. Baba yake alikuwa upande wa watawala wa kijeshi.

''Baba yetu, Kasa Hailu, alipigana na watoto wake wote watano,kisiasa lakini yeye na mimi tulipigana vita viitwavyo Adi Emiru.Alemtsehay Kasa alieleza.

Mama yake Alemtsehay alikuwa akiunga mkono waasi wa TPLF na kujaribu kumshawishi muwe wake, mwanajeshi, kubadili msimamo wake, alieleza.

Alimuandikia barua akimsihi mume wake kutopigana dhidi ya binti yao wa umri wa miaka 14- lakini alikataa na kuandika majibu akimtaka mkewe kumrudisha binti yao kutoka msituni.

Kisha Alemtsehay alimuandikia, akisema:

Nukuu: Utawala unaoupigania unawaua ndugu zetu na si wa kidemokrasia. Hata kama umejitoa, baba hapaswi kupigana na binti yake.''

Kwa mara nyingine alikataa kuiasi serikali, ambayo ilikuwa maarufu kwa vitendo vyake vya ''kigaidi'' ambavyo vilihgarimu maisha ya maelfu ya watu ambao walikuwa wakiupinga utawala.

Baadae bwana Kasa alijeruhiwa kwenye mapigano ya Feres kisha akashikiliwa mateka na waasi, hatimaye alifariki akiwa mateka mwaka 1982.

Alemtsehay Kasa alipanda cheo baada ya kuuangusha utawala wa Mengistu

Chanzo cha picha, Alemtsehay Kasa

Binti yake anasema aliposikia kuhusu kifo cha baba yake kutoka kwa wapiganaji wenzake ilimuathiri sana.

''Sikuweza kumuona baba yangu tena-nilihuzunika kusikia taarifa hiyo, zaidi ya hayo nilikwazwa sana kwa kuona kuwa baba yangu amekufa akiunga mkono utawala wa kidikteta na wenye kutekeleza mauaji''.Alieleza

Ilichukua miaka 17 kwa muungano wa waasi kuuangusha uongozi wa mtawala wa kijeshi Mengistu Haile Mariam ambaye alienda uhamishoni mwaka 1991.

Nduguze wawili pia waliuawa wakati wa vita.

Sasa akiwa kamishna wa polisi nchini Ethiopia na mama wa watoto wawili bi Almetshay anasema mbali na kuwa na maumivu ya kumpoteza baba yeke na nduguze, anajivunia nafasi aliyoitumia kumuondoa Mangitsu madarakani.