Wateja wa British Aiways walivyoathiriwa na tangazo la mgomo wa marubani

British Airways planes

Chanzo cha picha, PA Media

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mgomo wa mwezi ujao wa Shirika la ndege la Uingereza, British Airways unatarajiwa kusababisha siku tano ya kufutiliwa mbali wa safari za ndege.

Marubani wa British Airways wametangaza mgomo wa siku tatu utaofanyika kutoka tarehe 9. 10 na 27 mwezi Septemba kufuatia mzozo kuhusu nyongeza ya mshahara.

Licha ya mgomo wa kwanza kuwa Septemba 9 na 10 baadhi ya wasafiri waliokata tiketi za kusafiri kati ya tarehe 8 na 10 mwezio wameagizwa kufuta safari zao.

Lakini wateja wengine wanasema wamepokea ujumbe kupitia ujumbe wa Barua Pepe kimakosa.

Awali walifahamishwa kuwa usafiri wa ndege zao umefutwa, lakini baade wakaambiwa kuwa safari ipo.

Sarah Maxwell, kutoka Belfast, aliarifiwa kwa Barua Pepe kuwa ndege ya kutoka Dublin kwenda Dubai imefutwa -lakini alipopiga simu kwa wahudumu wa wateja wa shirika hilo alifahamishwa kuwa ndege hiyo itasafiri kama ilivyo pangwa.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya burudani Lizo Mzimba alijikuta katika hali kama ya Bi Sara Maxwell.

"Nimetumia muda mwingi kujaribu kufuatilia suala ambalo baadae lilibainika kuwa hitilafu ya kimitambo," alisema.

Shirika la Ndege la British Airways bado halijatoa tamko lolote kuhusiana na suala hilo.

'changamoto ya mawasiliano'

Baadhi ya wateja wamelalamikia changamoto ya mawasiliano na wahudumu wa BA iliwafanyiwe mpango mbadala wa usafiri.

British Airways iinawahudumia wasafiri 145 kila siku - ikiwa na ndege zaidi ya 280- kila baada ya sekunde 90 ndege ya shirika hilo inatua ua kupaa kutoka sehemu tofauti duniani.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Ndege la BA inasema: "Tunafanya kila tuwezalo tusivuruge mipango ya usafiri wa wateja wetu.''

Wateja wameripoti kupokea ujumbe usiku wa Ijumaa na Jumamosi saa zasubuhi kufahamishwa kuwa safari zao zimefutiliwa mbali.

Baadhi yao wametumia mitandao ya kijamii kulalamikia hatua hiyo wakisema wameshindwa kukata tena tikiti ya usafiri kupitia wavuti wa BA na kwamba simu wanazopiga haziwafikii wahudu sheirika hilo.

Presentational white space

Fungate 'zilizoathiriwa '

Abby Deem, 32,kutoka Cambridge anasema fungate yake''imevurugwa'' baada ya ndege yake kwenda Mauritius Mwezi Septemba tarehe 9 kufutiliwa mbali .

"Tumekuwa tukiikamia safari hii kwa mwaka mzima," alisema.

"Hakuna hata mmoja wetu aliyewahi kusafiri kwa kutumia usafiri wa ''business class'', na baada ya harusi tulifikiria ilikuwa wakati mwafaka wa kuanza fungate."

Ameelezea jinsi alivyovunjika moyo mchumba wake Jonathan walivyomtumia ujumbe kumfahamisha tukio hilo.

Wamelazimika kuabiri ndege nyingine ambayo itawagharimu £500 za ziada.

Abby Deem na mchumba wake Jonathan

Chanzo cha picha, Abby Deem

Maelezo ya picha, Abby Deem na mchumba wake Jonathan

Jennifer Bond, kutoka Manchester, alikuwa anatarajia kusafiri na mchumba wake Simon kuelekea Las Vegas kufunga ndoa lakini ndege yao kutoka Marekani (Septemba tarehe 11 na 25 September) zimefutiliwa mbali

Anasema: "Wamejiandaa kwa karibu miaka miwili alafu mipango hiyo inatibuka wiki tatu kabla ya safari."

Ilikuwa "vigumu" kufikia BA kwa simu, aliongeza kuwa walilazimika kununua tiketi ya ndege ya Virgin -iliyowagharimu £700 zaidi ya ndege ya awali.

"Tumeishiwa na hela na mchakato wa kurudishiwa pesa tulizotumia itachukua wiki nne," alisema.

Jennifer Bond na Simon Morris

Chanzo cha picha, Jennifer Bond

Maelezo ya picha, Jennifer Bond alikuwa anatarajia kurejea Las Vegas na mchumba wake kufunga ndoa

Mtaalamu wa usafiri wa angani Simon Calder anasema kuwa hatua ya kufutuliambali safari imetokana na msingi kwamba British Aiways haiwezi kutuma ndege , kwa mfano kwenda Hong Kong, ikiwa rubani atagoma siku itakayofuata.

Pia anasema BA haina budi kuwatafutia wateja wake usafiri mbadala siku hiyo hiyo hata kama itamaanisha ''iwanunulie tiketi katika ndege zingine''.

Ikiwa ndege itachelewa usiku kucha, anasema BA italazimika kugharamia malazi na chakula.

Chama cha marubani wa Shirika la Ndege la Uingereza (Balpa) kilisema siku ya Ijumaa wanchama wake hawana budi kugoma baada ya kuhangaishwa na wasimamizi wa Shirika hilo.

Marubani wa BA wamekataa nyongeza ya mshahara ya 11.5% kwa kipindi cha miaka mitatu, ambayo shirika hilo ilipendekeza mwezi Julai mwaka huu.

Anna Redding na mume wake Duncan Grist

Chanzo cha picha, Anna Redding

Maelezo ya picha, Anna Redding na mume wake Duncan Grist wanahofia safari yao ya kihistoria itavurugwa
line

Naweza kufanya kuomba kufidiwa ikiwa ndege yangu imeathiriwa na mgomo?

Arifa iliotolewa na na Shirika la ndege la British inasema kuwa mteja anaweza kuomba kurudishiwa pesa zake au kukata tiketi nyingine ya usafiri katika kipindi cha siku 355, ua kutumia gharama ya tiketi hiyo kusafiri sehemu nyingine.

Ikiwa ndege yako imefutiliwa mbali kwa sababu ya mgomo wa wafanyikazi wa shirika hilo mamlaka ya usafiri wa ndege nchini Uingereza linasema hatua itachukuliwa kulingana na sheria ya ndege hiyo.

Kuna baadhi ya wateja ambao pia watafidiwa kwa kuvurugiwa mipango ya safariI - lakini ikiwa wamepewa notisi ya ya kuwa safari yao imefutiliwa mbali chini ya siku 14.

line