Saudi Arabia yamuachilia mwanaufalme Khaled bin Talal baada ya mwaka mmoja kuzuizini

The Ritz Carlton in Riyadh on 11 Feb

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha, Wanaufalme walizuiliwa kwenye hoteli Ritz Carlton mjini Riyadh mwaka uliopita
Iliyochapishwa

Mwanaufalme ambaye alikamatwa kwa kukosoa opesheni dhidi ya ufisadi nchini Saudi Arabia anaripotiwa kuachiliwa huru kutoka kizuizini.

Jamaa wa Prince Khaled bin Talal walichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinaaminiwa kuchukuliwa wikendi hii zikionyesha mwanamke huyo akisalimiana na familia yake.

Mwanaufalme huyo ambaye amezuiliwa kwa karibu mwaka mmoja ni mpwa wa mfalme Salman.

Ndugu yake Khaled, Prince Alwaleed bin Talal alikuwa miongoni kwa wanaufalme kadhaa na watu wengine wa vyeo vya juu waliozuiliwa kwa ufisadi mwaka uliopita.

Hatua hii ya hivi punde inakuja wakati kuna shinikizo kubwa dhidi ya mwanaiufalme Mohammed bin Salman kufuatia kuuliwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.

Wadadisi wanasema mamlaka za Saudi Arabia zinajaribu kutuliza suala hilo kwa kutafuta uungwaji mkono kutoka familia ya kifalme.

"Asante kwa usalama wako, aliandika mpwa wake Khaled, Princess Reem bint Alwaleed, akichapisha picha zake akiwa na familia yake kwenye mtandao wa Twitter.

Picha zingine zilizochapishwa na watu wa familia zilionyesha mwanaufalme hiyo akimbusu mtoto mtoto wake wa kume amabaye amekuwa katika hali ya kupoteza fahamu kwa miaka kadhaa.

Serikalia ya Saudi Arabia haijatoa taarifa yoyote kuhusu kuzuiliwa au kuachiliwa kwake.

Lakini gazeti la Wall Street Journal liliripoti kuwa alizuiliwa kwa miezi 11 kwa kukosoa operesheni ya mwaka uliopita dhidi ya zaidi ya wanaufalme 200, mawaziri na wafanyabiashara kufuati madai ya ufisadi.

Walizuiwa kwenye mahoteli kwenye mji mkuu Riyadh ikiwemo hoteli ya kifahari ya Ritz-Carlton.

Hadi mwishoni mwa mwezi Januari mwendesha mashtaka nchini Saudi Arabia alisema zaidi ya dola bilioni 100 zilikuwa zimepatikana kutoka kwa wale waliokuwa wamezuiwa.