Njia mbadala za wanawake na wasichana masikini wakati wa hedhi

Tulimuomba mpiga picha Maisie Cousins kuelezea nini wanawake na wasichana hufanya wakati wanapokuwa kwenye siku zao za hedhi
Umasikini na kutokuwa na makazi au kasumba zinawalazimu wanawake na wasichana kuja na bidhaa mbadala za kujihifadhi za muda mfupi.
Hapa ni baadhi ya vitu ambavyo wanawake na wasichana hutumia badala ya vifaa vilivyozoeleka miaka yote.
Utafiti wa shirika la Plan International limebaini mwaka 2018.
Wakati pedi na taulo za wanawake zinapokuwa ghali, bidhaa yenye gharama nafuu ambayo huikimbilia ni karatasi za chooni

Asilimia 40 ya wanawake walio chini ya miaka 21 hutumia tissue wakati wa hedhi.
Baada ya tishu soksi ni ya pili kutumika.

Vitambaa, hufyonza damu ya hedhi na vinaweza kutumika tena baada ya kufua
Nguo kuukuu vilitumika sana, huku msichana mmoja akisema alilazimika kutumia Vesti kama pedi.

Pia magazeti na makaratasi yamekuwa yakitumika kama mbadala wa pedi.

Wakati mwingine hakuna la kufanya isipokuwa kujichafua tu kwenye nguo zao za ndani, wakiwa hawajavaa chochote.

Kwa wasichana hawa, njia ya kuvaa nguo za ndani zaidi ya moja hutumika kuzuia damu kutokeza nje.













