Mwamuzi wa soka wa Nigeria Joseph Ogabor afungiwa mwaka mmoja

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirikisho la soka Afrika, (Caf) imemfungia mwamuzi wa Nigeria, Joseph Ogabor kutojishughulisha na soka kwa mwaka mmoja kwa kosa la '' kujaribu kufanya udanganyifu kwenye mechi''.
Caf imesema uamuzi huo umekuja baada ya uchunguzi kufanyika na kupata ushahidi ambao uliwasilishwa kwa maafisa wa mechi hiyo nchini Afrika Kusini, ambao Ogabor aliwataka kutoa ''usaidizi wa kiufundi'' kwa timu ya Nigeria.
Plateau United ilitahadharishwa kujiepusha na vitendo vya ukarimu kama kutoa zawadi ambavyo vilionyesha kuwa na nia ya kutoa tafsiri mbaya.
''Shirikisho la soka la Afrika Kusini wameamriwa kuomba radhi kwa shirikisho la soka la Nigeria baada ya uchunguzi kuthibitisha kuwa hakuna ushahidi wa afisa yeyote wa shirikisho hilo kujihusisha na rushwa ya kiasi cha dola za Marekani 30,000''. ilihitimisha taarifa hiyo.








