Macron autetea mkataba wa Paris

Iliyochapishwa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameutetea mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabia ya nchi.

Amefanya hivyo katika hotuba yake, kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa, na katika ukumbi ambao mkataba huo ulisainiwa mjini New York, miaka miwili iliyopita.

Rais Macron amesisitiza kuwa hakutakuwa na kubadili msimamo juu ya makubaliano hayo katika wakati ambao sayari haiwezi kujadili, kwani amesema imeanza kulipiza kwa binadamu na kwamba matukio mabaya ya hali mbaya ya hewa yanaweza kuondesha tofauti kati ya nchi tajiri na masikini.

Ameahidi kutoa zaidi, dola bilioni tano kwa ajili ya Ufaransa kuwekeza katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

Katika hotuba yake hiyo pia aligusia mpango wa nyuklia wa Iran na kuitaka Myanmar kudhibiti mauaji yanayofanywa kwa kabila la Rohingya.

Ametoa wito pia wa hatua za kidiplomasia zichukuliwe katika kutafuta amani nchini Syria.