Wafungwa wakatwa vichwa ndani ya gereza Brazil

Wafungwa walionekana kwenye paa la gereza la Alcazuz

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wafungwa walionekana kwenye paa la gereza la Alcazuz
Iliyochapishwa

Polisi wa kukabiliana na ghasia nchini Brazil wanajaribu kila wawezavyo kuingia ndani ya gereza kuu katika jimbo la Rio Grande do Norte, ambalo limetwaliwa na wafungwa.

Idara ya olisi inasema kuwa, zaidi ya wafungwa kumi wameuwawa baadhi yao kwa kukatwa katwa katika makabiliano makali kati ya magenge hasimu katika gereza hilo la Alcaçuz.

Polisi hao wamefika nje ya ukuta wa gereza hilo wakisubiri hadi kutakapopambazuka ndipo waingia ndani.

Mwaka jana pekee zaidi ya wafungwa 100 wamefariki katika makabiliano kama hayo yaliyofanyika awali mwezi huu nchini humo katika magereza yaliyoko katika majimbo ya Amazonas na Roraima.

Polisi wanasema wanajaribu kudhibiti hali

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Polisi wanasema wanajaribu kudhibiti hali
Brazil
Maelezo ya picha, Brazil