Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mtoto aliyeibwa apatikana hai miaka 18 baadaye
Mtoto mchanga aliyeibwa katika hospitali moja ya jimbo la Florida nchini Marekani, amepatikana akiwa hai baada ya miaka 18 katika jimbo la South Carolina.
Kamiyah Mobley ,aliibwa kutoka kwa mamake akiwa na umri wa saa 8 pekee.
Mwanamke aliyejifanya kuwa muuguzi alisema mtoto huyo alikuwa mgonjwa na angehitaji uchunguzi wa kimatibabu.
Baadaye alitoweka na mtoto huyo.
Mwanamke anayeishi na mtoto huyo, Gloria Williams, ametiwa mbaroni baada ya polisi kupashwa ripoti.
Familia halisi ya mtoto huyo ilijuzwa taarifa kuhusu kupatikana kwake, baada ya uchunguzi wa vinasaba kubaini utambulisho wake.