Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mfalme Akihito wa Japan aomba kung’atuka
Mfalme wa Japan Akihito ameeleza mapenzi yake ya kutaka kung'atuka.
Akihutubia taifa hilo kupitia runinga, amesema ana wasiwasi kwamba umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.
Kwa sasa, hakuna nafasi kisheria kumruhusu mfalme kuondoka madarakani Japan.
Lakini muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema atathmini kwa makini matamanio ya mfalme huyo.
Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989.
Habari kwamba anataka kung'atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari mwezi jana.