Wiki ya Afrika katika picha:Novemba 2022

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaharakati wako nchini Misri kushawishi serikali na watunga sera kuchukua hatua juu ya mzozo wa tabia nchi , ambao unaathiri kwa kiasi kikubwa nchi maskini zaidi duniani.
Iliyochapishwa
th

Chanzo cha picha, WINSTON DUKE/GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Nyota Lupita Nyong'o, Tenoch Huerta, Danai Gurira na Winston Duke wakishiriki onyesho la kwanza la filamu la Wakanda Forever nchini Nigeria siku ya Jumapili...
TH

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mashabiki wapambwa nyuso zao na michoro iliyochochewa na filamu hiyo
TH

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwigizaji wa Algeria Sofia Boutella akiwa kwenye zulia jekundu katika hafla kwenye Jumba la Makumbusho la Sanaa la Kaunti ya Los Angeles siku ya Jumamosi.
TH

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Siku hiyo hiyo nchini Afrika Kusini, bendi inayoandamana inapita mbele ya Mbio za Mkokoteni za Red Bull.
TH

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Shindano huko Cape Town hushuhudia washiriki wakiendesha magari ya kujitengenezea nyumbani, sio yote ambayo yanafika utepeni
TH

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mshauri "Gogo" Shery Ziwakayi, kulia, akitoa kipindi cha ushauri bila malipo kwenye Benchi la Urafiki. Wazo hilo lilitoka kwa daktari wa magonjwa ya akili Profesa Dixon Chibanda, na Shirika la Afya Ulimwenguni sasa linaipeleka Qatar kwa Kombe la Dunia la kandanda.
TH

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku ya Ijumaa, mafunzo ya ballerina katika Ukumbi wa Grande wa Dakar nchini Senegal yamesimama karibu na picha ya mwalimu wa ballet wa Kirusi Agrippina Vaganova.
TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamume huyu hutengeneza sanamu ya ndege ,Gabe Bazaar huko Khartoum, Sudan, Jumamosi.
th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Siku moja kabla, mji mkuu ulikuwa mwenyeji wa michuano ya ulengaji shabaha
th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanawake hawa walengaji shabaha wanashiriki katika kitengo cha bunduki.
th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashabiki wa Esperance Sportive Tunis walipunga mkono kwenye mechi ya kuwania ubingwa wa Tunisia dhidi ya Union Sportive Tataouine siku ya Jumamosi.
th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Wanasiasa, mnaposimama kuzungumza, kizazi changu kinaomba mzungumze kama kuna dharura," Leah Namugerwa wa Uganda anasema katika hotuba yake kuu katika COP27...
th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbali na vituo vya mikutano na hoteli, maisha yanaendelea nchini Misri. Mwanamke huyu anakuza aina mbalimbali za mimea kwenye roshani yake kwa kutumia chupa za plastiki zilizorejeshwa.
th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Unaweza pia kuniua" ni kauli mbiu ya waandamanaji wa Ghana wanaopinga mzozo wa gharama za maisha nchini humo.
th

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Seun Kuti, mwana wa nguli wa Nigeria Fela, akitumbuiza katika tamasha la muziki la Villanos Del Jazz nchini Uhispania siku ya Jumatatu.
TH

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mvulana katika jiji la Lagos nchini Nigeria apata mguu mpya wa bandia, katika Kituo cha Uboreshaji cha Irede siku ya Jumatatu.
TH

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Pia siku ya Jumatatu, mamia ya watu waliojitolea walijiandikisha katika jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya rais wa nchi hiyo kutoa wito wa vijana kujiunga na jeshi kujilinda dhidi ya nchi jirani ya Rwanda.
TH

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Siku moja kabla, kumbukumbu za kuadhimisha urais wa miongo minne wa Paul Biya zinauzwa nchini Cameroon. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 89, ambaye ndiye rais mkongwe zaidi barani Afrika, hakuhudhuria sherehe za maadhimisho hayo.
TH

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Watu washiriki maandamano ya kupinga kukufuru huko Bamako, Mali, siku ya Ijumaa baada ya video ya mwanamume akiitusi Koran kusambazwa sana mtandaoni.
TH

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanariadha wa Kenya Sharon Lokedi asherehekea baada ya kushinda mbio za marathon za New York Jumamosi.
TH

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanaharakati wa Kenya Elizabeth Wathuti anazuru shamba la miti Arboretum Nairobi Jumanne.
TH

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Siku ya Jumatano mkulima anatayarisha ardhi msimu wa kupanda mahindi unapoanza nchini Zimbabwe.
TH

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Huku Kenya ikikabiliana na ukame unaozidi kuwa mbaya, ndovu hawa wanakunywa maji katika kituo cha maji kinachotumia nishati ya jua katika kaunti ya Taita Taveta.
th

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Na siku ya Jumatano, Mfalme Charles akisalimiana na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari katika Ikulu ya Buckingham mjini London.

Picha zote zipo chini ya hakimiliki.