Utoaji mimba nchini Marekani - nini kinafanyika?

Chanzo cha picha, Getty Images
Rebecca anakimbia mbele ya waandamanaji kwenda kwa mama wa watoto watatu, aliye peke yake kwenye kiti katika kliniki ya waavyaji mimba. Mwanamke huyo anaogopa kurudi kwenye kliniki, ‘Itakuwaje iwapo mtu ninayemjua kutoka kanisani kwangu ataniona?', anasema huku akitokwa na machozi. Kwa mkono mmoja Rebecca anakumbatia, na mwingine ananyoosha mwavuli wake ili kumkinga mwanamke huyo dhidi ya waandamanaji wanaopinga uavyaji mimba waliokusanyika nje.
Rebecca Rehm Tuggle alilelewa kama Mkatoliki nchini Marekani, sasa yeye ni msindikizaji wa watoaji mimba na amesimama nje ya kliniki ndogo katika jimbo la kusini la Louisiana. Yeye huwasaidia wateja kuepuka waandamanaji na kupata njia salama ya kuingia.
Hope Medical Group ndiyo kliniki pekee huko Shreveport, Louisiana na mojawapo ya tatu tu katika jimbo hilo, kwa takriban idadi ya wanawake 920,000 walio katika umri wa kuzaa (kati ya umri wa miaka 15 na 44).
Wagonjwa wanane kati ya kumi katika kliniki hii wanaishi chini ya umaskini na karibu asilimia 60 yao hujitambulisha kama Wamarekani wenye asili ya Kiafrika.
"Nilizungumza na mwanamke mmoja aliyekuja kutoa mimba jana, alisema ni vigumu kupata riziki kulingana na mambo yalivyo sasa. Siongelei pesa tu, nazungumzia muda - yeye ni mama, ana kazi mbili. na huwa anapata muda mchache na mtoto aliye naye nyumbani,” anasema Rebecca.

Chanzo cha picha, Rebecca Rehm Tuggle
Siku ya Ijumaa, uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Marekani ulibatilisha haki ya kisheria ya nchi nzima ya kutoa mimba ambayo ilikuwa imekuwepo kwa takriban miaka 50, na wengi kama Rebecca wana wasiwasi kuhusu athari ambayo hali hii mpya ya kisheria inaweza kuwa nayo kwa wanawake - hasa kwa wale wa jamii ndogo ambao hawajawakilishwa kwa njia isiyo sawa katika takwimu za uavyaji mimba.
Watu weusi ni asilimia 13 ya idadi ya watu nchini Marekani, lakini wanawake weusi hupokea zaidi ya theluthi moja ya ripoti za utoaji mimba nchini humo, na wanawake wa Hispanic karibu theluthi moja.
Wanawake maskini wana uwezekano mkubwa wa kutaka kuavya mimba, kulingana na takwimu , na wanawake wa makabila madogo wanaathiriwa zaidi na ukosefu wa usawa wa mali - huku pengo la utajiri kati ya makundi ya watu weupe na wasio wazungu likiongezeka katika miongo michache iliyopita.

Kwa sababu za umaskini
Katika tangazo lililotarajiwa kufuatia uvujaji wa mwezi uliopita, majaji wa Mahakama ya Juu ya Marekani walibatilisha uamuzi wa kihistoria wa mwaka 1973 uliojulikana kama Roe v Wade, ambao ulithibitisha vyema haki ya mwanamke ya kutoa mimba nchini Marekani.

Chanzo cha picha, Los Angeles Times via Getty Images
Taasisi ya Guttmacher, kikundi cha utafiti kinachounga mkono, kinatabiri kuwa utoaji mimba sasa unaweza kupigwa marufuku au kupunguzwa katika majimbo 26 - na kuathiri zaidi ya nusu ya watu walio katika umri wa kuzaa watoto.
Na wanawake maskini zaidi pamoja na wanawake wenye asili ya Kiafrika watabeba mzigo huo, kwani makundi haya yana uwezekano mkubwa wa kutaka kutoa mimba, kulingana na rekodi.

Kathaleen Pittman, ambaye anafanya kazi kama msimamizi wa kliniki huko Louisiana, anasema umaskini ndiyo sababu kuu ya wanawake kutoa mimba .
Wateja wengi ambao uhudumiwa na kliniki hulipia huduma hiyo na fedha kutoka kwa mashirika yasiyo ya faida.
"Tumekuwa na wagonjwa wanaotegemea ufadhili tatu tofauti wa utoaji mimba," anasema.
Kathaleen anahofia hali mbaya zaidi, sio tu kwa mustakabali wa kliniki yake na kazi yake: "Tutaenda kuona umaskini zaidi, vifo zaidi."
Kulingana na CDC, mnamo 2020 kiwango cha vifo vya uzazi kwa wanawake weusi wasio wa asili ya Hispanic kilikuwa juu mara tatu kuliko kiwango cha wanawake Wazungu wasio Hispanic.
Huko Louisiana, ni juu zaidi: wanawake weusi wana uwezekano wa karibu mara nne zaidi kuliko wanawake weupe kukumbwa na kifo kinachohusiana na ujauzito.
Utoaji mimba nchini Marekani - nini kinafanyika?
- Kufuatia rasimu ya maoni ya wengi iliyovuja kwa vyombo vya habari mwezi Mei, Mahakama ya Juu ya Marekani ilipiga marufuku haki ya kisheria ya nchi nzima ya kutoa mimba tarehe 24 Juni, kwa kubatilisha uamuzi wa kihistoria wa mwaka 1973 wa Roe v Wade.
- Uamuzi wa Mahakama ya Juu sasa unaruhusu mataifa kupiga marufuku utaratibu huo katika hatua za awali za ujauzito katika maeneo yao ya kisheria.
- Idadi ya uavyaji mimba iliongezeka kwa asilimia 8 katika kipindi cha miaka mitatu had mwaka 2020, na hivyo kurudisha nyuma takwimu zaa miaka 30 za kupungua kwa idadi, kulingana na data mpya iliyotolewa Juni.
- Jumla ya idadi ya watoa mimba nchini imepungua kwa kiasi kikubwa tangu miaka ya 1980 - ilikaribia kuwa nusu kati ya mwaka 1982 na 2017, kulingana na data ya Kituo cha Utafiti cha Pew.
Vita dhidi ya sheria
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kama Louisiana, majimbo mengine kadhaa tayari yalikuwa yamepata sheria za kupiga marufuku au kupunguza utoaji mimba mara tu baada ya kutangazwa kwa uamuzi wa Mahakama Kuu ya Marekani.
(LARTL) ni mojawapo ya mashirika kongwe na makubwa zaidi ya kupinga uavyaji mimba katika jimbo hilo. Kazi yake inahusisha kukuza kanuni za vizuizi ambazo serikali imekuwa ikipitisha katika miaka michache iliyopita, lakini pia kujihusisha na elimu, ushauri nasaha na uanaharakati, ikijumuisha vipindi vya maombi nje ya kliniki.
"Tunaamini kwamba haijalishi jinsi maisha yanavyotungwa, hata katika visa vya nadra na vya kutisha vya ubakaji na kujamiiana, maisha yanafaa kulindwa," anasema Sarah Zargorski, mkurugenzi wa mawasiliano wa LARTL.
Shirika lake linaamini kuwa matatizo ambayo wanawake walio wachache wanakabiliana nayo yanapaswa kushughulikiwa kwa kuunda upya mazungumzo kuhusu afya ya uzazi.
"Muda mwingi umetumika katika kile kinachoitwa huduma ya afya ya uzazi, lakini tuna fursa sasa kuzingatia huduma halisi ya afya ya uzazi."
LARTL hivi majuzi wameibuka na kusema wanapinga sheria yoyote ambayo inawza kumtia hatiani mama.

Chanzo cha picha, Valeria Perasso
Zaidi ya nusu ya watu weusi nchini Marekani wanaishi maeneo ya Kusini, ambako katika majimbo mengi wabunge tayari wameunda sheria au marekebisho ya kuzuia utoaji mimba kwa njia tofauti kwa miaka mingi - kwa mfano, kwa kuweka vipimo vya lazima vya uchunguzi, ushauri nasaha unaoelekezwa na serikali au vipindi vya kungojea kabla ya utoaji mimba.
Kwa Marcela Howell, rais na Mkurugenzi Mtendaji wa In Our Own Voice - ushirikiano wa kitaifa wa mashirika ya wanawake weusi yenye ajenda ya haki ya uzazi – ubatilishaji huo sasa unaonyesha wasiwasi mkubwa: "Sio tu kuhusu utoaji mimba, kwa wanawake weusi ni kuhusu uhuru wa mwili".
"Roe daima imekuwa sakafu na sio dari kwa wanawake weusi."
Anasema kwamba ingawa uamuzi wa Roe v Wade ulianzisha haki ya kutoa mimba, haujawahi kuondoa vikwazo vya kifedha wa wanawake weusi kutoa mimba, wala haukuzuia kanuni za serikali kufanya shughuli hiyo kuwa ngumu zaidi.












