Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Sitaki mtu mwingine yeyote atumie vitambaa kutengeneza pedi'
'Alikua kwenye kibanda'
Kazi yake imetambuliwa na jamii yake na aliteuliwa kwa orodha ya mwaka huu ya jarida la Forbes ya 30 under 30, ambayo inawaonyesha wanakampeni wenye umri mdogo na wajasiriamali kutoka kote ulimwenguni.
Akielezea malezi yake katika kitongoji cha Duncan Village katika jiji la London Mashariki, Tamara anasema ameishi maisha yake yote "kwenye kibanda - hawakuwahi kuwa na madirisha yoyote, wala maji [ya bomba]".
Aliamua kupata kazi za muda baada ya shule ili kujaribu kukimu mahitaji ya familia yake - na kusaidia alipokuwa kwenye hedhi.
"Nilianza kufanya kazi kila nilipoweza wakati ninasoma ili ninunue taulo za kusafishia nguo kwa sababu kwangu nguo hizo zilinisumbua sana."
Tamara pia anasema alipokuwa kijana alipata changamoto sana kuelewa kwa nini alikuwa anapata maumivu wakati wa hedhi, kwa sababu kulikuwa na elimu ndogo sana kuhusu hedhi.
Hakuwa peke yake katika changamoto hii.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya kupambana na Umaskini ‘The Borgen Project’ inakadiria kuwa wasichana milioni saba wa Afrika Kusini hawawezi kumudu kununua pedi.
Kote duniani, Benki ya Dunia inasema kuwa takriban wanawake na wasichana milioni 500 wanakosa huduma wanazohitaji wakati wa hedhi.
Shirika la Wanawake la UN linahesabu kuwa wanawake na wasichana bilioni 1.25 duniani kote hawana vyoo salama.
Na ndivyo ilivyo kwa Tamara na familia yake. Walitumia choo cha umma na wengine karibu 50 katika kitongoji chake.
Licha ya Afrika Kusini kuwa moja ya nchi tajiri zaidi barani, mfanyabiashara huyo mdogo anafikiri kuwa "inaangaza kutoka nje".
Alipoenda chuo kikuu cha Johannesburg kusomea mahusiano ya umma, Tamara alifanikiwa kuanza kuweka akiba ya pesa kutoka kwa mkopo wa mwanafunzi na pia mapato kutoka kwa kazi zake za muda ili kuanzisha biashara yake mwenyewe, akiwa na nia ya kubadilisha mambo kwa wanawake na wasichana katika jamii yake.
Ilibidi ajitegemee kwani alijaribu kupata mkopo wa biashara lakini hakuna mtu ambaye aliamua kumsikiliza licha ya mashaka mengi ya kuweza kulipa kwani hakuwa na mali yoyote kwa jina lake.
Hatimaye alizisha biashara hiyo mwaka wa 2021 kwa lengo la kuuza pedi au sodo kwa bei nafuu kwa wanawake wasiojiweza.
Aliliita Azosule, ambalo linamaanisha "kufuta kila chozi kutoka kwa macho yao" katika lugha ya Kixhosa ya Afrika Kusini.
Pia imekuwa kama shirika la hisani, kwa kutumia sehemu ya faida zake. Tamara alianzisha kampeni ya "Anakuhitaji" ambapo anaenda shule katika maeneo ya vijijini kupeleka pedi bure.
Mradi wa Borgen unakadiria kuwa karibu 30% ya wasichana katika maeneo hayo hawaendi shuleni wanapokuwa kwenye siku zao za hedhi kwa sababu ya kukosa pedi.
'Ilikuwa kama Krismasi'
Mwalimu wake mkuu wa zamani wa shule ya upili anajivunia kazi yake.
"Amewasaidia wasichana sana. Ameleta pedi nyingi sana ambazo wasichana wanazo za kutosha kwa miezi sita - ilikuwa kama Krismasi kwao," Thazea Mnyaka anasema.
"Wasichana hawa wanatoka katika familia maskini ambapo milo yao pekee inaweza kutoka shuleni, wanawezaje kununua pedi?"
Kwa kuongeza, Tamara anatoa pedi mitaani katika jamii zilizotengwa.
Yazini Kuse ni mwandishi wa habari, pia kutoka kijiji cha Duncan, na alikuwa mwandishi wa kwanza kuandika kile Tamara alikuwa akifanya.
"Nilivutiwa na kazi yake. Anatetea utu wa wasichana wadogo na haki za binadamu za wanawake kwa sababu hatuna mengi tunayoweza kufanya.
"Anajitahidi kurejesha hali hiyo," anaiambia BBC.
"Licha ya kuwa katika hali hiyo ya umaskini yeye mwenyewe. , anajaribu kuboresha maisha ya wengine, jambo ambalo linavutia- yeye ni ushuhuda muhimu kwa hili."
Kuna wengine nchini wanaoshughulikia suala hilo hilo.
Nokuzola Ndwandwe ni mwanakampeni kutoka Durban ambaye alifaulu katika hatua za kufutiliwa mbali ushuru wa mauzo ya pedi nchini Afrika Kusini, na anajitahidi kupata mswada unaozingatia bidhaa zinazotumika wakati wa hedhi.
Mswada wa Haki za Afya ya Hedhi unaungwa mkono na jumuiya ya mashirika 31 ambayo yanafanya kampeni ya bidhaa za bure na wanataka serikali ya Afrika Kusini kutambua afya ya hedhi kama suala la haki za binadamu.
Anasema: "Tulitaka [kodi] ifutwe kwa bidhaa za hedhi kwa sababu ni ghali. Tuko kwenye majadiliano na wanachama wakuu wa serikali na wanawake wa Umoja wa Mataifa.
"Ni muhimu kuwawezesha wanawake vijana kuchukua hatua. Wanawake na wasichana katika maeneo ya vijijini kama ya Tamara wanapaswa kuendelea kupaza sauti zao na kujitokeza."
Tamara ana malengo na anataka hatimaye kupanua kazi yake katika nchi nyingine za Afrika. Pia anataka wanaume watambue umuhimu wa kuvunja miiko.
"Hedhi ya Umaskini si suala la wanawake, ni suala la kijamii," anasema, "na hadi tuweze kuelewa hili hatutasonga mbele."