Sheria ya kijeshi aliyoweka Putin kwenye majimbo yaliyonyakuliwa kwa ukraine ina maana gani? 

Iliyochapishwa

Rais Vladimir Putin ameweka sheria ya kijeshi - kwa mara ya kwanza katika historia ya Urusi ya sasa, kwa sasa sheria hiyo inatekelezwa katika eneo pekee lililotwaliwa na Moscow.

Baraza la shirikisho liliidhinisha kwa kauli moja uamuzi wa Bw Putin. Rais mara moja alianzisha ''hatua''  mbali mbali za kiutawala katika majimbo ya Urusi yaliyosalia.

Magavana walipewa uwezo wa kuweka sheria mbali mbali katika maeneo yao.   Kwa mfano, matembezi ya wakazi katika maeneo yaliyo karibu na mipaka yanaweza kuzuiwa, magavana waliahidi kwamba marufuku ya aina hiyo haitawekwa kwa sasa.

Putin alitangaza kuanzishwa kwa sheria ya utawala wa kijeshi katika majimbo manne yaliyonyakuliwa na Urusi kutoka kwa Ukraine katika mwanzo wa mkutano wa baraza la usalama.   

Kremlin imekuwa ikizungumzia kuhusu hatua ya aina hiyo tangu Urusi ilipoishambulia Ukraine. Hatahivyo, maafisa wa Urusi wamekuwa wakisema kwa miezi mingi kwamba hakuna mpango wa kuweka sheria ya kijeshi  katika majimbo fulani au katika nchi nzima.

"Ngoja niwakumbushe kuwa Jamuhuri ya watu ya Donetsk, Jamuhuri ya watu wa Luhansk, pamoja na majimbo ya Kherson na  Zaporozhye zilikuwa chini ya sheria ya jeshi kabla ziwe shemu ya Urusi. Sasa tunahitaji kuanzisha utawala huu katika mfumo wa sheria ya Urusi. Hiyo ndio maana tulisaini sheria  juu ya kuanzishwa kwa sheria ya kijeshi katika maneo haya manne . Ninaiweka," alisema Putin.

Katika hotua yake, Rais huyo alizungumzia kuhusu "kura za maoni" ambapo kutokana na matokeo ya kura hizo ,maeneo ya Ukraine "yalijiunga na Urusi " ambazo na iwe Ukraine wala jamii ya kimataifa hawazitambui kuwa halali.  

 Sheria ya kijeshi nchini Urusi inadhibitiwa na sheria ya Urusi ya shirikisho iliyopitishwa katika mwaka 2002.

Kulingana na vipengele vyake, "uchokozi dhidi ya Shirikisho la Urusi au tisho la uchokozi la moja kwa moja " nisababu ya kuanzisha utawala wa aina hiyo.   

 Huku Putin akiweka sheria ya kijeshi, Ukraine inaimarisha mashambulio yake katika jimbo la Kherson.

Mamlaka zilizotwaliwa za jimbo zimeanza kuwaondoa wakazi wake pale, na kamanda  Sergei Surovikin, ambaye ndiye mkuu wa operesheni za kijeshi za urusi katika Ukraine, anasema kwamba kuna "hali ngumu katika  Kherson" na kwamba haitakuwa rahisi kuchukua uamuzi. 

Sheria ya kijeshi inawapa maafisa haki isiyo na ukomo kuzuia uhuru wa watu , kuweka majimbo katika hali ya usimamizi wa jeshi.

Kipengele cha 7 cha sheria ya shirikisho "kuhusu Sheria ya Kijeshi’’ inaelezea hatua zinazochukuliwa. 

  • Mfumo maalumu wa kuingia na kutoka katika eneo lililotangazwa kuwa chini ya sheria ya kijeshi, kudhibiti matembezi pale
  • Kuwazuia wananchi kuondoka Urusi
  • Kuzuia maadamano yaliyoandaliwa, mikusanyiko, na migomo
  • Ujasusi wa kijeshi – mkiwemo kufuatilia mazungumzo ya sim una mawasiliano
  • Kuzuia shughuli za vyama na mashirika (ikiwa ni pamoja na mashirika ya kidini) kuhusika na propaganda na vitendo vinavyoweza kusababisha wasi wasi na fujo
  • Kununua mali na taifa ya matumizi ya taifa (ambazo hutolewa kwa mmiliki wa mali baadaye katika mnada)
  • Haki ya kuzuia matembezi magari  na kuyakagua
  • Kuanzisha hamri ya kutotoka nje nyakati za usiku
  • Kuzuia mauzo ya silaha, utawala maalumu kwa  ajili ya mauzo ya vilevi, na madawa
  • Kuwaajiri raia katika kazi za ulinzi – kwa mfano, kujenga upya majengo mapya ya jeshi yaliyoharibika
  • Kuwahamishia wakazi kwenye "maeneo salama".
  • Kuzuia kutoka  (kulazimishwa kujitenga, kuhamishwa au kudhibitiwa kwa uhuru wa kutembea ) kwa raia wa nchi iliyomo vitani na Urusi (kwa sasa Ukraine). 

Maelezo ya kipengele cha 7 yanaonyesha kuwa kuzuiwa kwa watu kutoka kwenye maeno yao kwa hali ya sasa kumefanyika kwa msingi wa uchokozi dhidi ya Shirikisho la Urusi.

"Kuwekwa kwa ''sheria ya kijeshi'' na Urusi  katika maeneo yaliyonyakuliwa kunapaswa kuchukuliwa kama uamuzi ambao unahalalisha kisheria uporaj iwa mali ya Ukraine kabala ya "uhalisho" ujao. Alisema mkuu wa ofisi Mikhail Podolyak.

 

"Hatua nyingine "

 

Zaidi ya kunyakuliwa kwa majimbo manne, amri ya  Putin pia iliyataja majimbo mengine. Aya ya tatu ya waraka wa amri hiyo  inasema kuwa "ikiwa muhimu"hatua nyingine zitachukuliwa" zinazotolewa atika sheria yam waka 2002.

Kipengele cha sheria kinaangaliwa sana, hasa kwasababu hakiko wazi ni mamlaka gani kinachoipatia mamlaka na ni wapi kitatumiwa.

Hakuna maelezo ya "hatua nyingine" katika sheria. "Hatahivyo, Kipengele cha  8 of Sheria ya kijeshi inaelezea "hatua nyingine"  ambazo maafisa wanaweza kuzianzisha ili  "kutengeneza bidhaa"au kutoa huduma kwa ajili ya mahitaji ya taifa, jeshi na watu.

Sergey Krivenko, mkuu wa shirika la haki za binadamu "Raia. Jeshi.Sheria " (walijumuishwa katika sajiri ya mashirika ya kigeni nchini), anaamini kwamba Putin anatekeleza kwa uhalisi kipengele nambari 8, hata kama haielezwi bayana katika waraka. 

Miongoni mwa "hatua nyingine" zilizoainishwa katika kipengele nambari ni haki ya mamlaka ya kuweka masharti  kuhusu ‘’shughuli za kiuchumi na ", ununuzi wa mali, uhuru wa mauzo ya bidhaa na huduma, ukusanyaji  na usambazaji wa habari.  

Sheria pia inasema kwamba "hatua nyingine" inaweza kutumiwa sio katika majimbo  ambako kumewekwa sheria ya kijeshi, lakini pia katika maeneo mengine ya nchi.