Kurunzi ya Qatar 2022: Yafahamu mataifa matano yanayopigiwa chapuo kutwaa ubingwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Hizi ni taarifa kubwa kuhusu kombe la dunia jioni hii
1. Haya ni mataifa 5 yanayopigiwa chapuo Qatar
Brazil haijatwaa kombe la dunia tangu mwaka 2002, lakini mashindano ya mwaka huu ya Qatar 2022, yanaweza kubadili hali hiyo.
Brazil, mshindi mara tano wa kombe la dunia anapewa kipaumbele kwa kupata asilimia 16%, huku ikipewa nafasi kubwa ya kuingia fainali (25%).
Nyuma ya Brazil, ni Argentina yenye Lionel Scaloni (13% ) na ya tatu ni kwa kupewa nafasi ya nne ni Ufaransa (12%), Hisapnia (9%) na England (9%).
2. Mataifa yameanza kuwasili Qatar

England imewasili Qatar usiku wa Jumanne kuelekea fainali za kombe la dunia zinazoanza Jumapili. Kikosi cha watu 26 cha Gareth Southgate kilipaa kikitokea Birmingham.
Wales, Tunisia, Senegal, Iran, Korea Kusini na Australia ni miongoni mwa mataifa yaliyowasili yakiendelea na maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya kuanza kwa fainali hizo.

Chanzo cha picha, AFP
3. Hiki ndicho kikosi chenye thamani kubwa zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiosi cha England kinaongoza kwa thamni, kikiwa na thamani ya £1.31bn huku kiungo wake Jude Bellingham akiwa ni mchezaji mwenye thamani zaidi, kwa mujibu waCIES Football Observatory.
England imezipiku Brazil (£1.27bn) iliyoshika nafasi ya pili, Ufaransa ya tatu kwa thamani (£1.17bn) na ya tano ni Hispania (£1.05bn).
4. Hatuogopi kusema tutatwaa ubingwa Qatar
Nahodha wa England Harry Kane, ametamba kikosi cha three Lions kitatwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka huu.
Kane anasisititza kwambva ' hatuogopi' kusema. England mara ya mwisho kutwaa kombe la dunia ni mwaka 1966.

Chanzo cha picha, Getty Images












