Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 28.07.2024

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Kiungo wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, ameiambia Manchester City kuwa anataka uhamisho wa kudumu kutoka kwa klabu hiyo, huku Everton na Aston Villa zikizingatia mkataba wa mkopo. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Nigeria Kelechi Iheanacho, 27, anakaribia kujiunga na Sevilla baada ya mkataba wake na Leicester City kumalizika. (Sky Germany)

Paris St-Germain bado wana nia ya kumsajili winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 22. (RMC - kwa Kifaransa)

Aston Villa inataka kumnunua mshambuliaji wa Barcelona na Brazil Raphinha, 27, msimu huu (Football Insider)

Liverpool na Tottenham wameungana na Arsenal katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26, kutoka Sporting Lisbon. (Football Insider)

Arsenal na Chelsea wako tayari kuwania saini ya mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Julian Alvarez, 24. (TeamTalk), kutoka nje.

Mkataba kati ya Aston Villa na Atletico Madrid kumhusu mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 24, haujakamilika bila pendekezo rasmi lililotumwa kwa klabu hiyo ya Uhispania. (Fabrizio Romano)

Newcastle italazimika kulipa euro 40m (£33.73m) kama wanataka kumsajili beki wa kati Mjerumani Malick Thiaw, 22 kutoka AC Milan. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Leicester City na Southampton watavutiwa na mshambuliaji wa Liverpool na Scotland Ben Doak, 18, ikiwa klabu hiyo itamweka kwa mkopo. (Athletic- Usajili unahitaji)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi