Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 03.05.2024
Manchester United wako mbioni kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Michael Olise, 22. (ESPN)
Juventus wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mashambuliaji wa Manchester United na Uingereza Mason Greenwood, 22, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Getafe ya Uhispania. (i Sport)
Kocha wa Barcelona Xavi ameiambia klabu hiyo kwamba anamtaka kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 29, lakini Bayern Munich pia wanamtaka. (Sport - kwa Kihispania)
Chelsea wanafikiria kumnunua mlinda lango wa Poland Wojciech Szczesny, 34 - mlinda mlango wa zamani wa Arsenal ambaye sasa anachezea Juventus. (Tutto Juve - kwa Kiitaliano)
Chelsea wameungana na Newcastle kuulizia hali ya mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Tosin Adarabioyo, 26, ambaye ataondoka Fulham kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)
Manchester City walikuwa miongoni mwa timu zilizomchunguza beki wa Borussia Dortmund Mholanzi Ian Maatsen, 22. (TBR Football)
Mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 27, yuko tayari kupigania nafasi yake katika klabu ya Arsenal huku kukiwa na tetesi zinazoashiria mchezji huyo anaweza kuondoka majira ya kiangazi. (Sun)
Meneja wa Brighton Roberto de Zerbi asalia kwenye orodha ya kocha wa Bayern Munich baada ya Ralf Rangnick kukataa ofa ya klabu hiyo ya Ujerumani. (Bild - kwa Kijerumani)
Leicester City wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Coventry City Muingereza Callum O'Hare, 26. (Football Insider)
Beki wa kati wa Aston Villa na Brazil Diego Carlos, 31, ni mmoja wa walengwa wakuu wa AC Milan. (Team Talk)
Brighton, Fulham, West Ham na Benfica wanamfuatilia winga wa Vitoria de Guimaraes na Ureno Jota Silva, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 17. (Rudy Galetti)
Villa wanataka kumsajili shambuliaji wa Leicester na Nigeria Kelechi Iheanacho, 27, kama mshambuliaji msaidizi wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Ollie Watkins, 28. (Football Insider)
Inter Miami wameanza mazungumzo na winga wa Benfica mwenye umri wa miaka 36 na Argentina Angel di Maria. (ESPN Ajentina - kwa Kihispania)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi