Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi Vita vya Urusi vilivyowapokonya nguvu matajiri wa Ukraine
Kwa miongo kadhaa, wafanyabiashara matajiri wakubwa wa Ukraine wamekuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi na kisiasa ndani ya nchi yao.
Hata hivyo, tangu uvamizi wa Urusi, viongozi wa wafanyabiashara maarufu zaidi wa Ukraine (oligarchs) wamepoteza mabilioni ya mapato.
Je utawala wa oligarchs wa Ukraine umefikia mwisho?
Mtu tajiri zaidi wa Ukraine, Rinat Akhmetov mwenye umri wa miaka 56 kwa wengi ni mfano wa oligarch.
Mtoto wa mchimbaji wa makaa ya mawe aligeuka kuwa bilionea wa kujitegemea, anajulikana kote Ukraine kama "Mfalme wa Donbas."
Pamoja na kumiliki sekta kubwa ya chuma na makaa ya mawe upande wa mashariki, ikiwa ni pamoja na kiwanda cha chuma cha Azovstal ambacho sasa kimeharibika, pia anamiliki Shakhtar Donetsk FC, mojawapo ya timu bora za soka nchini, na hadi hivi karibuni ana miliki moja ya TV kubwa zaidi nchini humo.
Lakini zaidi ya utajiri wao mkubwa, oligarchs wa Ukraine pia wanajulikana kwa kutumia mamlaka ya kisiasa.
Mnamo mwaka 2017, washauri wa uchumi na siasa kutoka nyumba ya Chatham ambayo iko mjini London walisema kuwa kuna"hatari kubwa zaidi kwa Ukraine".
Kupitia mtandao mkubwa wa washirika na wabunge waaminifu, oligarchs wa Ukraine wameathiri mara kwa mara upitishaji wa sheria kwa manufaa ya biashara zao.
Rais Volodymyr Zelensky aliwaita "kundi la watu wanaofikiri wao ni muhimu zaidi kuliko wabunge, maafisa wa serikali au majaji".
Lakini kwa raia wengi wa kawaida, tangu mwanzo wa uvamizi wa Urusi mashariki mwa Ukraine mnamo 2014, biashara zao zilisambaratishwa na makombora na mali zao kupotea kwa uvamizi wa Urusi.
Wengi waliona kwamba mtu tajiri zaidi wa Ukraine Bw Akhmetov alipaswa kufanya jitihada zaidi tangu mwanzo kukomesha uharibifu uliochochewa na Urusi katika ukanda wake.
Wakati ushawishi wa Urusi ukisaidiwa na nguvu za kijeshi ukienea huko Donbas, aliwaambia wafanyakazi katika viwanda vyake kupiga ving'ora vyao ili kupinga.
Lakini kuhusu kufadhili na kuunga mkono upinzani, alikosolewa kwa kuchukua hatua ndogo sana. Hasa ikilinganishwa na tajiri mwingine wa Ukraine, bilionea Ihor Kolomoisky.
Mnamo Machi 2014, aliteuliwa kuwa gavana wa Mkoa wa Dnipropetrovsk, kusini-mashariki mwa Ukraine.
Mzozo ulipozidi, Bw Kolomoisky alitoa mamilioni katika vikosi vya kujitolea vya Ukraine.
Aliwalipa kwa kuwakamata wanamgambo wanaoungwa mkono na Urusi na kulipatia jeshi la Ukraine mafuta.
Hata hivyo mnamo mwaka 2019, alijikuta akishindwa kukubaliana na mtangulizi wa Rais Zelensky, Petro Poroshenko.
Bunge lilikuwa limepitisha sheria hivi karibuni ambayo ilisababisha Bw Kolomoisky kupoteza udhibiti wa kampuni ya mafuta.
Majibu yake yakawa? Kwenda katika makao makuu ya kampuni ya mafuta wakiwa na watu wanaodaiwa kuwa na bunduki.
Lakini vita vilipoendelea mashariki, na kutokana na kupotea kwa viwanda vingi zaidi, migodi na mashamba yenye rutuba, kuangamia kwa matajiri wakubwa wa Ukraine ulikuwa ukiendelea.
Pigo lililofuata lilikuja mwishoni mwa 2021, wakati Ukraine ilipitisha kile kilichojulikana kama "muswada wa kupambanana na ubwenyenye".
Sheria mpya ya Rais Zelensky ilifafanua oligarch kama mtu ambaye alikidhi masharti matatu kati ya manne yafuatayo:
- Kuwa na ushawishi katika vyombo vya habari au siasa
- Kugharamia usambazaji wa bidhaa na huduma
- Kutengeneza mamilioni ya dola kwa mwaka.
Wale wote waliopitishwa walipewa fedha za ziada na kupigwa marufuku kufadhili vyama vya siasa.
Ili kuzuia kuwekwa kwenye orodha ya Zelensky, Rinat Akhmetov ingeweza kuuza mara moja mali zake zote za vyombo vya habari.
Lakini baadaye kukaja kuongezeka kwa mzozo kwa Urusi - uvamizi wa Ukraine mnamo Februari 2022.
Vita hivyo vimezidisha upotevu wa mapato kwa matajiri wakubwa wa Ukraine. Lakini je, kuanguka kwao kutaimarisha demokrasia ya Ukraine?
"Hakika," anasema Sevgil Musayeva, mhariri mkuu wa tovuti maarufu ya habari inayofahamika kama ‘Ukrainska Pravda.’ "Vita hivi ni mwanzo na mwisho wa oligarchs nchini Ukraine."
"Sheria ya kuondolewa kwa matajiri wakubwa ilikuwa mojawapo ya vichochezi vya kwanza vya kuangamia kwao," anasema Serhiy Leshchenko, aliyekuwa mmoja wa waandishi wa habari mashuhuri wa uchunguzi wa Ukraine na sasa mshauri wa mkuu wa wafanyakazi wa Rais Zelensky.
"Lakini vita vilipozidi, vilifanya maisha ya oligarchs kuwa magumu zaidi," ameiambia BBC. "Wamelazimika kuzingatia kufanikiwa kwao badala ya siasa za nyumbani."
Kwa sasa, anasema Bi Musayeva, ni juu ya mashirika ya kiraia ya Ukraine na taasisi za kupambana na rushwa kuzuia kuibuka kwa oligarchs wapya. Na, kwa hakika, uhai wa demokrasia nchini Ukraine unategemea matokeo ya vita na Urusi.