Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (05.08.2022)

Iliyochapishwa

Rais wa Corinthians Duilio Monteiro Alves amethibitisha kuwa klabu hiyo ya Brazil ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. 

Ronaldo, ambaye alirejea United takriban mwaka mmoja uliopita akitokea kwa wababe wa Italia, Juventus, anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto kwa ajili ya kutafuta taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. United walimaliza katika nafasi ya sita kwenye Premier League msimu uliopita, hivyo watashiriki Europa League msimu huu. 

Manchester United wamesikitishwa na kucheleweshwa kupita kiasi kwa mkataba wa muda mrefu wa Frenkie de Jong huku kukiwa na masuala ya kifedha ya Barcelona. 

Manchester Evening News imefahamishwa kwamba United wamekubali ada ya jumla ya €85million (£71.5m) kwa De Jong lakini kuahirishwa kwa majadiliano ya  mishahara kwa kiungo huyo kunaendelea kuzuia uhamisho kukamilishwa. 

De Jong, 25, anadai takriban €17m katika mishahara ambayo haijalipwa kutoka Barcelona kuanzia Novemba 2020 wakati wachezaji wa Barcelona walipokubali kukatwa mishahara yao ili kupunguza mzozo wa kifedha wakati wa janga la Covid-19 . 

Everton na Lille wanaendeleza mazungumzo kuhusu uhamisho wa kiungo Amadou Onana. 

Onana alisajiliwa na Lille kutoka Hamburg kwa €7m (£5.9m) msimu uliopita ili waweze kupata faida kubwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyecheza mechi 11 na akitokea benchi 21 kwenye Ligue 1 ya Ufaransa msimu uliopita. 

Wakati huo huo, dili la kumrejesha Gueye Goodison Park kutoka Paris Saint-Germain liko katika hatua ya mwisho na muhimu ambapo dalili zote za kurejea klabuni hapo zimeonekana. 

Chelsea imetangaza usajili wao wa tano wa beki wa pembeni wa Brighton Marc Cucurella majira ya kiangazi. 

Cucurella anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa majira ya kiangazi katika kikosi cha kwanza baada ya Raheem Sterling, Kalidou Koulibaly, Gabriel Slonina na Carney Chukwuemeka. Inafahamika kuwa kitita kamili cha pauni milioni 63 kimetumika kuipata sahihi yake. 

United na Chelsea wataendelea kumfuatilia Denzel Dumfries kulingana na ripoti za michezo. 

Dumfries, 26, alihama kutoka PSV Eindhoven kwenda Inter Milan msimu uliopita, lakini tayari anaweza kuondoka. Ripoti zinaonyesha kuwa Inter wameweka bei ya pauni milioni 34 kwa mchezaji huyo wa kimataifa mwenye mechi 35 na kwamba kuna uwezekano wa fedha hiyo kuongezeka kutokana na sheria za FFP.