Tetesi za soka Ulaya Jumapili 18.08.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Joe Gomez aliachwa nje ya kikosi cha Liverpool wakati wa ushindi wa Jumamosi dhidi ya Ipswich huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akitafuta uhamisho, huku Newcastle, Aston Villa, Fulham na Chelsea zote zikionesha nia ya kumtaka mlinzi huyo wa Uingereza. (Times)
Liverpool haitazamii kumuuza Gomez, huku bosi Arne Slot akiwa na furaha kwa mchezaji huyo kupambana na kurejea kwenye ushindani. (Liverpool Echo)
Mkufunzi wa Fenerbahce Jose Mourinho yuko tayari kuwasiliana na klabu ya zamani ya Tottenham kuhusu dili la kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Giovani lo Celso, 28. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa, Roma na Real Betis pia wanavutiwa na Lo Celso ambaye ameambiwa hayupo kwenye mipango ya mkufunzi wa Tottenham Ange Postecoglou na anaweza kuondoka kwa takribani £13m. (Fichajes)
Kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 33, amewaambia maafisa wa Barcelona kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo, mwaka mmoja tu baada ya kusajiliwa kutoka Manchester City kwa uhamisho wa bure. (Sport )
Wolves wako kwenye vita na Fenerbahce, Sevilla na Marseille kumsajili winga wa Uhispania Ansu Fati, 21, kwa mkopo kutoka Barcelona. (Sport )
Mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, 27, bado anaweza kuondoka Everton kabla ya dirisha la usajili kufungwa huku mkufunzi wa Toffees Sean Dyche akitamani kusajili kiungo na winga mwingine. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanajiandaa kumpa kiungo wa kati wa Uhispania Rodri nyongeza ya mshahara wake mara mbili, na kuongeza mshahara wake wa wiki hadi pauni 375,000, ili kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 katika klabu hiyo. (Sunday Mirror)
Mlinda lango wa Georgia Giorgi Mamadashvili, 23, anatamani kuhamia Liverpool na klabu ya sasa ya Valencia itamruhusu aondoke watakapokuwa wamepanga mbadala wake. (Football Espana)
Manchester United wana nia ya kuwashinda Liverpool katika kumsajili Mamadashvili, lakini kwanza wanahitaji kupunguza kikosi chao na kuongeza fedha kwa kumuuza winga wa Uingereza Jadon Sancho, 24. (Mirror)
Mlinzi wa Poland Jakub Kiwior anaweza kuondoka Arsenal kabla ya kumalizika kwa dirisha la uhamisho lakini hakuna mikataba iliyofika kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich wako tayari kutoa ofa kwa kiungo Leon Goretzka ingawa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 29, anataka kusalia na kupigania nafasi yake. (Florian Plettenberg)
Chelsea ilijaribu kumsajili mshambuliaji wa Italia Federico Chiesa, 26, kutoka Juventus katika mkataba wa kubadilishana Raheem Sterling, 29, lakini uhamisho huo ulivunjika kwa sababu ya mshahara wa mlinzi huyo wa Uingereza. (Gianluca Di Marzio)
Winga wa Watford kutoka Colombia Yaser Asprilla, 20, hatajiunga na klabu ya La Liga ya Girona, huku Porto wakiwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsajili. (Sport)












