Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je umewahi kusikia jua likigongana na jua jingine?
Wataalamu wa anga za juu wamegundua kugongana kwa jua kwa jina nyota za neutron kupitia darubini yenye uwezo mkubwa sana.
Mgongano huo ni muhimu katika kuuelewa ulimwengu.
Inaaminika kutengenezwa vyuma vizito vilivyounda nyota na sayari kama zetu mabilioni ya miaka iliopita.
Mwangaza kutoka kwa mitetemeko inaonekana kwa usiku kadhaa tu, kwa hivyo lazima darubini iende mbio ili kuipata.
Wanaastronomia waliona mgongano mmoja kama huo mwaka wa 2017, lakini waliurekodi kwa bahati tu.
Darubini kubwa ya Transient Optical Gravitational-Wave Observer (GOTO) iliojengwa na Uingereza, na ambayo ipo juu ya mawingu kwenye kisiwa cha Uhispania cha volkeno cha La Palma, sasa itazitafuta kwa utaratibu .
"Ugunduzi mzuri unapobainika , kila mtu atashughulika ili kutumia fursa hiyo zaidi," Profesa Danny Steeghs kutoka Chuo Kikuu cha Warwick aliniambia kwenye La Palma.
"Kasi ni muhimu. Tunatafuta kitu kinachojitokeza kwa muda mfupi sana, hachukua muda mfupi kabla ya kupotea," aliongeza.
Nyota za nyutroni ni nzito sana kwamba kijiko kidogo cha nyenzo zao kina uzito wa tani bilioni 4.
Darubini hiyo inaruhusu wanaastronomia kufungua mojawapo ili kuona kilicho ndani.
Ili kuweza kuona vizuri anga, darubini huwekwa juu ya mlima , eneo lenye kila aina ya darubini kila moja ikiwa inachunguza matukio tofauti.
Inapofunguka, hufichua betri mbili za jeti-nyeusi za darubini nane za silinda zilizounganishwa pamoja, miundo inayofanana zaidi na virusha roketi hatari.
Kila betri husimamia sehemu ya anga juu yake, ikizunguka kwa kasi na wima.
Tafuta eneo iliopo
Nyota ya nyutroni ni jua lililokufa na kuangukia uzito wake mkubwa , na hivyobasi kuvunja atomu zilizolifanya kung’ara.
Nyota hizo huwa mvuto mkubwa hatua inazozifanya kuvutana . mara nynegine hugongana na kushikana.
Wakati hilo linapotokea, husababisha mwangaza mkubwa na tetemeko la ardhi Hilo hufanya kila kitu kilichopo duniani kutingisika.
Mtikiso huo uharibu anga. Wakati unaponguliwa duniani, darubini mpya huanza kufanya kazi kutafuta eneo ulipotokea mwangaza huo.
Wanaonedesha darubini hiyo huutafuta katika kipindi cha masaa, ama hata madakika baada ya kugundua mtetemeko huo.
Hupiga picha ya anga na kuziondoa kidijitali nyota, sayari na galaksi ambazo zilikuwepo usiku uliopita.
Madoa yoyote ya mwanga ambayo hayakuwepo hapo awali yanaweza kuwa yanagongana na nyota za neutroni.
Hii kawaida huchukua siku kadhaa na wiki, lakini sasa lazima ifanyike kwa wakati halisi. Ni kazi kubwa ambayo inafanywa kwa kutumia programu.
"Unaweza kufikiria milipuko hii ni ya nguvu sana, yenye kung'aa sana, na kwamba inapaswa kuwa rahisi," profesa wa unajimu Joe Lyman, "lakini lazima tutafute nyota milioni 100 kwa kitu kimoja kinachotuvutia."
"Tunapaswa kufanya hivi kwa haraka sana kwa sababu kitu hicho kitatoweka ndani ya siku mbili," alisema.
Kugundua ulimwengu
Kundi hilo linashirikiana na wanaastronomia wengine kuchunguza mgongano huo kwa undani zaidi.
Mara tu wanapotambua mgongano huo, wanageukia darubini kubwa na zenye nguvu zaidi kote ulimwenguni. Hizi zinaonyesha mgongano kwa undani zaidi na kwa urefu tofauti wa mawimbi.
Utaratibu huu "unazungumza juu ya fizikia kwa ukamilifu," Lyman alisema.