Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Matukio 10 ya kukumbukwa mwaka 2022 kuhusu vita vya Ukraine
Tunaingia mwaka mpya. Lakini mapigano nchini Ukraine hayajaisha. Na siku chache kabla ya Krismasi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anazuru Marekani ili kujadiliana na Rais Joe Biden na kuhutubia Bunge la Marekani pamoja na tukio jingine muhimu.
Ikiwa ni kuhesabu tu matukio muhimu yaliyotokea katika uwanja wa vita katika vita vilivyodumu kwa zaidi ya miezi 10 sasa, kuna mengi katika vita vikali kwa pande zote.
Mashambulizi ya Ukraine na uondoaji wa vikosi vya Urusi Ikiwa pamoja na mashambulizi mengi makubwa ni vitu vya kukumbukwa.
BBC Thai imekusanya matukio 10 muhimu tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi wa Ukraine mnamo Februari 24 hadi sasa tukiumaliza mwaka 2022.
Urusi kuondoa vikosi vyake katika miji kuzunguka Kiev
Baada ya Urusi kuanza uvamizi kamili wa Ukraine mnamo Februari 24, ilielekea katika miji mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kiev. Baadhi ya wanajeshi wa Urusi walivuka mpaka wa Belarus kaskazini mwa Kiev na kuingia Ukraine. Lakini miezi michache tu ikipita, Jeshi la Urusi halikuweza kumaliza vita, na kuamua kuondoa wanajeshi kutoka miji inayozunguka Kiev. ikijumuisha Jiji la Irbin na Jiji la Ibada.
Baada ya kuyaondoa majeshi yake ikageukia kushambulia eneo la Don Bas upande wa mashariki mwa Ukraine.
Kuzama kwa meli ya kivita ya The Moscow
Tukio lingine kubw alililotokea lilikuwa ni meli ya kivita ya Moscow. Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, meli ya kusafirisha makombora Moskva, ambayo ilishambuliwa na mlipuko mnamo Aprili 14, ilizama katika Bahari Nyeusi.
Ukraine inadai kuishambulia kupitia kombora la A Neptune . Ikiwa madai hayo ni ya kweli basi meli hiyo ya kivita ya Urusi itakuwa ya kwanza kubwa kuzama tangu vita vya pili vya dunia.
Kutekwa kwa mji wa bandari wa Mariupol
Urusi ilitumia zaidi ya miezi miwili kujaribu kuuteka mji wa bandari wa Mariupol kwenye pwani ya Bahari ya Azov. Ni eneo muhimu kimkakati kuunganisha peninsula ya Crimea iliyounganishwa na Urusi na sehemu ya mashariki ya Ukraine.
Baada ya mapigano makali hasa karibu na Kiwanda cha Chuma cha Azovstal ambacho ni ngome ya upande wa Ukraine, hatimaye Urusi ilisonga mbele, kushinda katikati ya mweiz Mei.
Mamia ya wanajeshi wa mwisho mwisho wa Ukraine walijificha chini ya kiwanda hiki cha chuma kwa wiki kadhaa bila kuona mwanga, huku wakiishiwa chakula na maji na kulazimika kujisalimisha mwishowe.
Wanajeshi hawa walijificha kwenye handaki lililoko kwnye kiwanda lenye ukubwa wa mita za mraba 10 ambalo lilitengenezwa kusaidia watu kujikinga na vita vya nyuklia.
Fungua njia za mizigo katika Bahari Nyeusi.
Ukraine ni muuzaji muhimu wa nafaka nyingi nje ya nchi ikiwa ni pamoja na mafuta ya alizeti, ngano na mahindi. Kufungiwa kwa bandari za Urusi kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi nchini Ukraine na kukasababisha bei ya vyakula kupanda juu duniani kote na uhaba mkubwa wa chakula katika baadhi ya nchi maskini zaidi duniani.
Ndani ya miezi michache ya vita, kulikuwa na takriban tani milioni 20 za nafaka ambazo Ukrainia ilitaka kuuza nje, zilisalia nchini humo.
Uturuki ikafanya mazungumzo na Urusi na Ukraine kuhusu kufungua "njia ya baharini" katika Bahari Nyeusi ili kuruhusu mizigo kusafirishwa kwa usalama kwa njia ya meli. Hatimaye pande hizo mbili zilikubaliana na kutia saini, na mnano Agosti 1, 2022, njia ilifunguliwa.
Kuondoa vikosi katika miji ya mashariki
Baada ya Urusi kuelekeza mashambulizi yake katika mikoa ya mashariki ya Ukraine. Ikakutana na ugumu mwingine mnamo Septemba. Ukraine iliwazidi nguvu wanajeshi wa Urusi ikawalazimu warusi kuondoa wanajeshi kutoka miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na Kupiansk, Izum, Balaklya, na Kharkiv. Upande wa Urusi ulisema “Hawakutoroka. Urusi baadaye ilithibitisha kuwaondoa wanajeshi katika "jaribio la kuimarisha" eneo la mbele huko Donetsk. Imeutwaa tena mji wa Izum na mji wa Kupiyansk.
Urusi kuajiri wanajeshi wapya 300,000
Muda mfupi baada ya kurudi Urusi ilichukua hatua kubwa. Rais Vladimir Putin alitangaza uhamasishaji mkubwa wa kuajiri wanajeshi 300,000 katikati mwa mwezi Septemba. Lazima uwe na ujuzi maalum unaohitajika kupigana kwenye vita Ukraine. Wanajeshi hawa wa akiba ni pamoja na maofisa wa akiba wengi ambao baadhi yao wana zaidi ya miaka 60 na wamestaafu. Ilikuwa uhamasishaji wa kwanza mkubwa wa Urusi kufanyika tangu Vita vya pili vya dunia.
Kufanyika kwa kura ya maoni kuunganisha mikoa minne
Wakati huo tangazo la uhamasishaji wa wanajeshi wapya wa akia Urusi likiendelea, nchi hiyo pia ikakimbilia kufanya kura ya maoni kuhusu kuitwaa mikoa minne ya Ukraine: Donetsk, Luhansk, Zaporizhia na Kherson.
Inatajwa ni kura ya maoni "feki" ambayo si ya uaminifu na inakiuka sheria za kimataifa. Kisha, mwishoni mwa Septemba, Rais wa Urusi alitangaza Rasmi kunyakua mikoa hiyo minne ya Ukraine na kuwa sehemu ya Urusi.
Kushambuliwa kwa daraja la Crimea
Mashambulizi kwenye daraja la Crimea sehemu ya Peninsula ya kusini ya Ukraine, ambayo ilikuwa imetwaliwa na Urusi mwaka 2014, lilikuwa tukio kubwa la Oktoba 8, wakati bomu lilipolipuka kwenye daraja hilo linalounganisha Crimea na Urusi.
Upande wa Urusi umeshutumu Ni kazi ya mikono ya upande wa Ukraine. Lakini Ukraine haijadai kuhusika na shambulio hilo.
Daraja hili lenye urefu wa kilomita 19 kwenye Mlango-Bahari wa Kerch ndilo pekee linalounganisha barabara na reli ya moja kwa moja kati ya Crimea na Urusi.
Linasifiwa na vyombo vya habari vya Urusi kama "ujenzi wake ni wa karne" na ukitumia bajeti ya takriban baht bilioni 115. Umuhimu wa daraja hili ni katika usambazaji wa silaha na askari wa Kirusi kusini mwa Ukraine.
Kushambuliwa kwa miundo mbinu muhimu ya Ukraine
Kushambuliwa kwa daraja la Crimea Ilitumiwa na Urusi kama kisingizio cha kushambulia miundombinu na huduma muhimu za Kiukreni kote nchini.
Urusi ilianza kushambulia gridi ya nishati ya Ukraine mnamo Oktoba 10 baada ya kushindwa katika vita kadhaa nchini Ukraine. Mwishoni mwa Oktoba, Urusi ilifyatua wimbi jingine la makombora katika maeneo yote ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na Kiev.
Matokeo yake, 80% ya Kiev haina umeme na maji ya bomba. Kushambulia miundombinu ya nishati ni sehemu ya mkakati wa kuzima ari ya Ukraine kabla ya majira ya baridi kali ambayo joto hupungua hadi nyuzi 20 Celsius, na kuwaacha mamilioni ya watu bila maji huku wakikabiliwa na giza na baridi kali.
Kuondoa wanajeshi kutoka Carzon
Tukio lingine muhimu katika vita hivi lilikuwa Kuondolewa kwa askari wa Urusi kutoka mji wa Kherson, kusini mwa ukraine.
Ni mji pekee wa kikanda wa kati nchini Ukraine ambao Urusi imeushikilia tangu mwezi, huku wanajeshi wa Urusi wakiondoka hatua kwa hatua hadi Novemba 10 na kuunganisha nguvu ng'ambo ya mto Dnieper.
Ras Vladmir Putin ameamuru kuondolewa kwa vikosi vya Urusi katika mji wa Kherson, jambo ambalo hata wachambuzi limewashangaza. Na hilo linachukuliwa kama kushindwa vikubwa kwa Urusi.
Baada ya vikosi vya Urusi kuondoka, wanajeshi wa Ukraine waliingia mjini nkatika mji huo na kukaribishwa kwa furaha na wakazi na kushsherehekewa kwa furaha. Rais Zelensky pia alitembelea mji huo.
Hivi majuzi, mnamo Desemba 24, askari wa Urusi walianzisha shambulio lingine kwenye mji wa Kherson. Kulingana na serikali ya Ukraine makombora 41 yalirushwa kutoka ukingo wa kushoto wa Mto Dnieper, na kuua watu 11 na kujeruhi kadhaa. Raia walilazimika kuhamishwa kutoka Carzon tena.