Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Chelsea wanataka dau la £ 100m kwa Jackson

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Chelsea waweka dau kubwa kwa Nicolas Jackson, Barcelona wamgeukia Marcus Rashford katika kumsaka winga mpya wa kushoto, Juventus wakubali kima fulani kwa ajili ya Jadon Sancho na mengine mengi.

Chelsea imeweka dau la pauni milioni 100 kwa mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, huku AC Milan ikimtaka. (Mail)

.

Chanzo cha picha, Reuters

Mchezaji wa Manchester United na Muingereza Marcus Rashford, 27, anafuatiliwa na Barcelona kama winga mpya wa kushoto baada ya klabu hiyo ya Uhispania kushindwa kumnunua mshambuliaji wa Liverpool na Colombia Luis Diaz, 28, na Mhispania mwenye umri wa miaka 22 Nico Williams wa Athletic Bilbao. (Sky Sports)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus wamekubaliana mkataba wa euro 20m (£17.3m) na Manchester United kumnunua winga wa Uingereza Jadon Sancho, ambaye anafanya mazungumzo na klabu hiyo ya Old Trafford kabla ya uhamisho wowote. (La Stampa - in Italian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham bado wanavutiwa na mchezaji wa kimataifa wa DR Congo Yoane Wissa, licha ya kuwa hawajawasiliana na Brentford baada ya kuambiwa kuhusu thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuwa £50m mapema msimu huu wa joto. (Standard)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

PSV Eindhoven wako tayari kumuuza winga wa Ubelgiji Johan Bakayoko, 22, huku Everton, Nottingham Forest na Bournemouth, pamoja na RB Leipzig na Bayer Leverkusen, wakionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Nottingham Forest inaweka dau la pauni milioni 25 pamoja na nyongeza kwa kiungo mshambuliaji wa England chini ya umri wa miaka 21 James McAtee lakini Manchester City wameweka thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuwa karibu pauni milioni 40. (Mail)

Atalanta wanataka ofa ya angalau pauni milioni 50 ili kufikiria kumuuza beki wa kati wa Italia Giorgio Scalvini, 21, ambaye anasakwa na Newcastle United na Manchester United. (i paper)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal bado wanammezea mate winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, licha ya wao kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Muingereza Noni Madueke, 23. (GiveMeSport).

Aston Villa wanakaribia kukamilisha dili la mlinda lango wa Uholanzi Marco Bizot mwenye umri wa miaka 34 kutoka Brest ya Ufaransa. (Athletic - subscription required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Klabu ya Uturuki Fenerbahce inakaribia kupata dili la kumsaini kiungo mshambuliaji wa Uhispania Marco Asensio, 29, kutoka Paris St-Germain. (Football Italia)

Winga wa Colombia Daniel Munoz, 29, anatumai kuondoka Crystal Palace msimu huu wa joto licha ya kusaini kandarasi mpya mwezi Aprili pekee. (Mirror)