Je, ni nini kilichosababisha mzozo kati ya Papa Francis na viongozi wa Marekani wenye msimamo mkali dhidi ya mageuzi yake?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Mvutano kati ya Papa Francis na kikundi chenye nguvu cha kihafidhina cha Kanisa Katoliki nchini Marekani umeongezeka.

Papa Francis aliamua wiki zilizopita kumfukuza kadinali Mmarekani Raymond Leo Burke kutoka kwa makazi yake huko Vatican na kumnyima mshahara wake.

Alifanya hivyo wiki tatu tu baada ya kumfukuza mkosoaji mwingine mkali ambaye alipinga mbinu na mageuzi yake: Joseph Strickland, ambaye alikuwa askofu wa Tyler, Texas.

Vitendo hivi viwili vinawakilisha mabadiliko mapya katika mapambano ya kiitikadi kati ya Papa, ambaye anakuza maono ya wazi zaidi na jumuishi la Kanisa Katoliki, na sekta za kihafidhina za taasisi hiyo, ambazo zimejitolea kutumia kikamilifu mafundisho yake na mawazo ya jadi.

Kardinali Burke

Raymond Burke, mtu mashuhuri katika Kanisa Katoliki, amemkosoa papa Francis waziwazi mara kadhaa, akijiweka kama mtu mkuu wa upinzani wa kihafidhina ndani ya taasisi hiyo.

Upinzani wake wa sauti kwa mipango mbalimbali ya upapa, hasa wale wanaotetea mageuzi ya kimaendeleo, pamoja na kutokubaliana kwake na mtazamo wa kimaendeleo wa papa kwa mafundisho na utendaji wa Kanisa, vimekuwa chanzo kikuu cha mvutano miaka hii iliyopita.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kardinali Burke

Burke, mwenye umri wa miaka 75, amepinga waziwazi mtazamo wa Vatikani kwa masuala kama vile msimamo wake kuelekea jumuiya ya LGBTI - waziwazi zaidi chini ya upapa wa Francis - au jukumu la walei katika masuala ya kanisa.

Alishiriki pia katika vuguvugu la Kikatoliki la kihafidhina ambalo lilipinga waziwazi uongozi ulioanzishwa.

Kwa kujibu, Francis aliamua kumfukuza kutoka kwa nyumba yake ya Vatican na kuondoa mshahara wake, hatua ambayo haijawahi kufanywa katika muongo wa upapa huyo kutoka Argentina.

"Burke aliadhibiwa baada ya miaka 10 ya kumnyanyasa Francis na kujaribu kujiweka kama mamlaka ya maadili ya juu kuliko papa," mwanatheolojia na mwanasheria wa Marekani Dawn Goldstein, ambaye ni mtaalamu wa Kanisa Katoliki, aliiambia BBC Mundo.

Chanzo kimoja cha habari cha Vatican, kwa upande wake, kilieleza kuwa uamuzi huo haujumuishi adhabu ya mtu binafsi na unatokana na imani kwamba mtu hafai kufaidika na marupurupu ya ukardinali kwa kumkosoa kiongozi mkuu wa Kanisa.

Askofu Strickland

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Papa Francis na Strickland wakati wa mkutano mnamo 2020.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tarehe 11 Novemba, Papa Francis alimuondoa Askofu Joseph E. Strickland kutoka Dayosisi ya Tyler, Texas, baada ya kukataa kujiuzulu kufuatia uchunguzi wa Vatican.

Uchunguzi huo ambao ulifichua dosari katika usimamizi wa fedha wa Strickland, ulihitimisha kwamba hafai kuendelea na wadhifa huo.

"Hakuna uhalifu uliopatikana, ni usimamizi mbaya tu. Askofu mwingine yeyote, hangeondolewa," anasema Goldstein.

Kwa mwanatheolojia, sababu halisi ya kutimuliwa kwa askofu ilikuwa upinzani wake wa wazi kwa Francis.

"Siyo tu kwamba Strickland alikuwa akisimamia vibaya dayosisi yake, pia alikuwa akitumia muda mwingi kwenye mtandao akiwataka waumini wampuuze Papa na kumshutumu papa kwa kudhoofisha amana ya imani, ambayo ni imani iliyopitishwa na Yesu kupitia mitume. ” anaeleza.

Goldstein anasema kuwa kutoa shutuma kama hiyo "kwa kweli ni kutangaza mgawanyiko kwa heshima na papa."

"Na, ikiwa pia alikuwa msimamizi mbaya, inaeleweka kabisa kwamba Papa alitaka Strickland aondoke," anahitimisha.

Akiteuliwa na hayati Papa Benedict XVI mnamo 2012, Strickland alianzisha mfululizo wa mashambulizi dhidi ya majaribio ya papa kubadili msimamo wa Kanisa kuhusu masuala ya kijamii na ushirikishwaji kama vile uavyaji mimba, haki za watu waliobadili jinsia na ndoa za jinsia moja.

Kasisi huyo amekuwa akijishughulisha sana na mitandao ya kijamii, mara nyingi akiitumia kama jukwaa kuelezea kutokubaliana kwake na mkuu wa sasa wa Vatikani.

Wiki hii tu, kasisi huyo alitangaza kufungua chaneli yake ya YouTube ambapo kuna uwezekano atajaribu kuongeza maoni yake juu ya Ukatoliki.

Papa Francis

Ikumbukwe kwamba, hatua za kinidhamu alizochukua Papa Francis dhidi ya Kardinali Burke na Strickland ni za kiutawala na si za uhalifu. Wala hajashtakiwa kwa uhalifu.

"Lakini wote wawili walionyesha kwa njia yao wenyewe kwamba hawakufanya kama inavyofaa askofu, aliyeitwa kutenda tu kwa muungano na Papa, kamwe dhidi yake," Goldstein alisema.

Na anaongeza kuwa "jibu bora itakuwa toba na unyenyekevu kwa kila askofu, kwa ajili ya umoja wa Kanisa chini ya papa. Lakini iwapo hilo litafanyika au la itategemeana Burke pamoja na Strickland ".

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Papa kisha aliwakosoa waziwazi wahafidhina.

Vyovyote vile, Papa Francis anazidi kuonyesha wazi upinzani wake kwa sekta za kihafidhina za Kanisa Katoliki.

Papa alinyooshea kidole cha lawama moja kwa moja kwa uonozi wenye msimamo mkali wa taasisi hiyo nchini Marekani wakati wa mkutano na Wajesuiti kwenye mkutano wa vijana wa Kikatoliki mjini Lisbon (Ureno) mwezi Agosti.

"Nchini Marekani, hali si rahisi: kuna tabia kali sana ya misimamo mikali . Imepangwa na kuunda mali ya watu, hata kihisia," alisema.

"Ulienda Marekani na unasema ulihisi hali ya hewa iliyofungwa. Ndio, hali hii ya hewa inaweza kupatikana katika hali fulani, "aliwaambia watazamaji.

Naye alisema kwamba “itikadi inapochukua nafasi ya imani, kuwa mwanachama katika sehemu fulani ya Kanisa kunachukua nafasi ya kuwa mshiriki wa Kanisa.”

Papa aliwaalika wakosoaji wake kuelewa kwamba "kuna mageuzi sahihi katika uelewa wa maswali ya imani na maadili" na kwamba "haina maana" kuangalia nyuma.

Kwa mfano, alidai kwamba karne nyingi zilizopita, baadhi ya mapapa walistahimili utumwa.

Maoni ya aina hii yamechochea, miongoni mwa wahafidhina wakubwa wa Kanisa, kutoamini sana - hata upinzani wa wazi - kwa viongozi wake.

Msimamo mkali wa Marekani

Kadinali na askofu aliyeidhinishwa na papa wanaambatana na msimamo mkali unaozidi kuwa na nguvu ndani ya Kanisa Katoliki nchini Marekani.

Katika nchi hii yenye wakazi zaidi ya milioni 330, Wakatoliki wanawakilisha karibu 20% ya wakazi na, kulingana na tafiti, kuna uwiano fulani kati ya idadi ya waaminifu kwa nafasi za maendeleo na wale wanaotetea mawazo ya kihafidhina.

Daraja la kikanisa la Marekani linaundwa na maaskofu 434 hai na waliostaafu, wakiwemo makadinali 16.

Na inazidi kuwa, uongozi wa juu wa Kanisa Katoliki nchini humo unashikilia msimamo mkali, ukitetea mafundisho ya kitamaduni ya taasisi hiyo dhidi ya majaribio ya Vatikani ya kurekebisha maadili chini ya uongozi wa papa wa Argentina.

"Sijui ikiwa wale wanaompinga Francis ni wengi, lakini wana nguvu zaidi na wamedhibiti Mkutano wa Maaskofu wa Marekani kwa miaka mingi," asema Dawn Goldstein.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakatoliki wasio na imani msimamo mkali nchini Marekani wanapinga kikamilifu, miongoni mwa mambo mengine, utoaji mimba na ndoa za jinsia moja.

Wahafidhina hawa huchukua msimamo mkali kuhusu masuala kama vile ngono, ndoa za watu wa jinsia moja, udhibiti wa kuzaliwa na uavyaji mimba.

Na, ingawa kwa kawaida wanaunga mkono mamlaka ya upapa, kwa miaka mingi wamemkosoa mkuu wa Kanisa kwa mielekeo wanayoona kuwa ya huria sana, hasa kuhusu kujumuika na kukabiliana na hali halisi ya kijamii. masuala ya kisasa kama vile matibabu ya jamii ya LGTBI.

Pia wanatofautiana na Francis kuhusu masuala kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, uhamiaji, haki ya kijamii, udhibiti wa bunduki na hukumu ya kifo.

Goldstein anaeleza kuwa ni kundi lenye nguvu sana, linaloungwa mkono na ulimwengu wa biashara na ambalo linadhibiti mtandao mkubwa wa vyombo vya habari ambamo linakuza mawazo yake na ukosoaji wake kwa Papa.

"Wamekuwa wakifanya kazi kwa miaka mingi, hasa Marekani, ili vyombo vyao vya habari viwe wasemaji wa Wakatoliki na hivyo kwamba simulizi yao ni hadithi iliyoidhinishwa," anaeleza mwanatheolojia huyo.

Anasema kuwa, miongoni mwa masuala mengine, suala ambalo bado lina utata la uavyaji mimba lilichukua nafasi ya msingi katika kuleta itikadi kali kwa wasomi wa Kikatoliki wa Marekani.

Ingawa Kanisa Katoliki kwa ujumla linajitangaza kuwa "linalounga mkono maisha" au kupinga uavyaji mimba, msimamo wa kiitikadi wa kuunga mkono haki ya wanawake ya kuchagua umeunganishwa ndani ya Chama cha Kidemokrasia cha Marekani.

Hii, kulingana na Goldstein, iliruhusu Chama cha Republican cha kihafidhina kujiweka kama mtetezi wa Wakatoliki na kujiimarisha, kwa kuungwa mkono na Maaskofu wa kihafidhina, kama mshirika mkuu wa kisiasa wa Kanisa, na kuzipendelea taasisi hizo mbili kupatanisha itikadi zao na nafasi za maadili.

Imetafsiriwa na Seif Abdalla