Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 05.04.2024
Mshambuliaji wa Ureno Joao Felix anasema mchezaji mwenzake wa kimataifa Bernardo Silva, 29, anataka kuhamia Barcelona, huku kiungo huyo wa kati wa Manchester City akihusishwa na klabu hiyo ya Catalan mara kadhaa hivi majuzi. (Gerard Romero)
Liverpool wameanza mazungumzo na mkufunzi wa Sporting Lisbon Ruben Amorim, 39, kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp huko Anfield. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)
Barcelona pia walikuwa wanamtaka kocha huyo wa Ureno lakini wamesitisha mpango huo kwani wanafikiri huenda akaelekea Liverpool. (Sport - kwa Kihispania)
Manchester United wanafikiria kumnunua mlinzi wa Aston Villa wa Uingereza Ezri Konsa, 26. (Footbal Transfers)
Atalanta wanasema hawajapokea mawasiliano yoyote ya moja kwa moja kutoka kwa Liverpool kuhusu kiungo wao Mholanzi Teun Koopmeiners huku Reds wakiripotiwa kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (90 min)
Liverpool wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Uruguay Federico Valverde, 25, kutoka Real Madrid. (Team Talk)
Mshambuliaji wa Bologna na Uholanzi Joshua Zirkzee, 22, amekuwa akinyatiwa na Manchester United na Liverpool, lakini amemwambia wakala wake angependelea kuhamia AC Milan. (Mirror)
Arsenal wanajiandaa kupambana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Barcelona mwenye umri wa miaka 19 Mikayil Faye. (Calciomercato, via TeamTalk)
Manchester United imempa mkataba mpya winga Mwingereza Bendito Mantato mwenye umri wa miaka 16 huku klabu kadhaa maarufu zikimtaka kinda huyo. (Fabrizio Romano)
Klabu ya Everton huenda wakapunguziwa pointi kwa mara ya tatu baada ya ripoti ya akaunti zake za hivi punde kutolewa. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi