Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 05.10.2024.

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United itafufua mazungumzo na mkufunzi wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel iwapo watamfukuza Ten Hag. (ipaper).

Uongozi wa United utakutana Jumanne kujadili masaibu ya klabu hiyo baada ya mmiliki mwenza Sir Jim Ratcliffe kuwatazama wakicheza na Aston Villa kwenye Ligi ya Premia Jumapili. (Athletic - subscription required)

Mkufunzi wa Inter Milan Simone Inzaghi amekataa ofa ya kumrithi Ten Hag katika Old Trafford (Sportitalia - in Italian)

Kocha wa zamani wa Manchester United Rene Meulensteen anasema atakuwa tayari kurejea ikiwa Ruud van Nistelrooy, meneja msaidizi kwa sasa katika klabu hiyo, angekuwa meneja. (No Tippy Tappy Football Podcast, via Mirror)

Real Madrid wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, 20. (Football Insider)

Arsenal wanavutiwa na mshambuliaji wa Barcelona mwenye umri wa chini ya miaka 19 wa Barcelona Arnau Pradas. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester City wamemjadili kiungo wa kati wa Crystal Palace na Uingereza Adam Wharton, 20, kama kiungo mbadala wa Rodri aliyejeruhiwa. (Football Insider)

Everton itajaribu kufufua mazungumzo ya kandarasi mpya na mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 27, ikiwa mapendekezo ya kutwaa umiliki wa Friedkin Group yatakubaliwa. (ipaper)

Liverpool wana nia ya kumsajili fowadi wa Uingereza Eberechi Eze, 26, kutoka Crystal Palace. (Football Insider)

Barcelona na Atletico Madrid zote zinapanga kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Ghana Thomas Partey, 31. (Fichajes, via TeamTalk)

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi