Tetesi za soka Ulaya Jumamosi  06.08.2022

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Barcelona wamesalia kwenye mazungumzo na Chelsea kuhusu beki wa kushoto wa Uhispania Marcos Alonso na wana uhakika wa kufikia makubaliano ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.  (90min)

Alonso amewaaga wafanyakazi katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea wa Cobham huku akitarajia kukamilisha uhamisho wake wikendi hii. (Mail)

Crystal Palace wana nia ya kumsajili tena beki wa pembeni wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka, 24, kutoka Manchester United. (Sky Sports)

Everton wanajiandaa kushinda West Ham katika kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Amadou Onana, 20, kutoka Lille.  (Mirror)

 

th

Chanzo cha picha, Getty Images

 

Chelsea huenda ikalazimika kuvunja rekodi ya ada ya uhamisho ya £80m kwa beki - inayoshikiliwa na Harry Maguire - ili kumsajili beki wa kati wa Ufaransa Wesley Fofana, 21, kutoka Leicester City. (Telegraph)

Tottenham wanapanga kukamilisha dili na Udinese kumnunua beki wa Italia Destiny Udogie, 19, wiki ijayo.  (Fabrizio Romano)

Leeds wanalenga mkataba wa pauni milioni 22 kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Arnaud Kalimuendo, 20. (Sun)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, yuko tayari kusalia na klabu hiyo ya Uhispania kwa mshahara uliopunguzwa licha ya Chelsea na Manchester United kumtaka. (Sport - in Spanish)

Mazungumzo "yamesalia wazi" kati ya Manchester United na Red Bull Salzburg kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Slovenia mwenye umri wa miaka 19 Benjamin Sesko.  (Sky Sports)

Mmiliki wa Leeds Andrea Radrizzani amesema Chelsea ilikubali ada ya £65m kumnunua Raphinha kabla ya "ushawishi wa Barcelona" kumfanya  winga huyo wa Brazil, 25, kuchagua kujiunga na klabu hiyo ya Uhispania badala yake.  (The Athletic)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea imemsajili beki wa Uhispania Marc Cucurella kutoka Brighton kwa mkataba wa thamani ya zaidi ya £60m.

Beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 24, ambaye alifunga bao moja katika mechi 38 katika msimu wake pekee akiwa na Seagulls, amesaini mkataba wa miaka sita.(BBC Sport)

Kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona Cesc Fabregas amemtaka fowadi wa Argentina Lionel Messi, 35, kuondoka Paris St-Germain na kurejea Nou Camp.  (Mirror)

Middlesbrough wanakamilisha dili la kumsajili fowadi wa Marekani Matthew Hoppe, 21, kutoka Mallorca.  (90min)