'Jamii imekuwa ikitutazama kama watu tusioweza, nataka waone uwezo na sio ulemavu'

'Jamii imekuwa ikitutazama kama watu tusioweza, nataka waone uwezo na sio ulemavu'
Iliyochapishwa

Mshiriki wa kwanza wa Tanzania kwenye mashindano ya ulimbwende kwa walemavu wanaotumia kiti mwendo ngazi ya dunia mwaka 2022 Witness Raphael anasema licha na changamoto kadhaa ikiwemo kushambuliwa mitandaoni hakukataa tamaa na shabaha yake ni kunyakua taji hilo na kuleta mabadiliko ya kifikra kwa wasichana wenye ulemavu nchini Tanzania.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Oktoba 23 hadi 29 2022 kwenye jiji la Tijuana na Rosarito nchini Mexico lengo likiwa ni kuonesha uwezo walionao wasichana wenye ulemavu na kuhimiza ushirikishwahi kwenye jamii katika nyanja mbalimbali Shindano hili lilifanyika kwa mara ya kwanza 07.10.2017.

Katika shindano la mwaka Witness atachuana na walimbwende wengine kutoka duniani yakiwemo mataifa ya Afrika kama vile Afrika Kusini, Nigeria, Kenya na Cameroon.

Eagan Salla ametuandalia taarifa ifuatayo.