Hali ya isiyo ya kawaida inayomfanya mtu kudumaa na kuonekana kama kijana mdogo

.

Chanzo cha picha, PERSONAL FILE

Iliyochapishwa

Luiz Augusto Márcio Marques, 23, maarufu Guto, alikuwa kama mtoto wa kawaida hadi alipofikisha umri wa miaka 7 huko Passo Fundo, kusini mwa Brazil.

Kuanzia wakati huo na kuendelea, alianza kuwa na maumivu makali ya kichwa na, baadaye aligunduliwa kuwa na uvimbe isiyo ya kawaida kwenye ubongo - hali ambayo huathiri mtu mmoja tu kati ya watu milioni moja.

Akiwa na umri wa miaka 8, Guto alilazimika kufanyiwa upasuaji kuondoa sehemu ya uvimbe huo. Lakini hatua hiyo ilikuwa hatari: huenda angepoteza uwezo wa kuzungumza, kuona, kutembea na hatimaye ukuaji wake pia ungeathiriwa.

Na mwisho hicho ndicho kilichotokea. Katika hali nadra sana, mvulana huyo aliacha kukuwa alipofikisha umri wa miaka 12 hivi.

"Nilifanyiwa upasuaji la sivyo ningekufa baada ya siku chache"

Guto aliendelea kuumwa na kichwa mara kwa mara na maumivu yalizidi kuwa makali, lakini hakuna hata mmoja kati ya madaktari waliyomhudimiwa aliyeweza kumtambua ratizo lilikuwa wapi.

“Nilianza kupata kuumwa na kichwa nikiwa shuleni, sikuweza kusoma na baadhi ya madaktari walisema nina tatizo la kisaikolojia, uvivu, wengine walisema ni virusi tu,” alisema.

L

Chanzo cha picha, PERSONAL FILE

Ni baada ya Guto kupata kifafa na kupelekwa hospitali ya jiji ndipo ambapo waliweza kugundua alichokuwa nacho: craniopharyngioma.

“Kisha wakamwambia shangazi yangu kwamba ilikuwa hatari, na kupendekeza nifanyiwe upasuaji la sivyo nitakufa baada ya siku chache,” anasema.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ndani ya ubongo wa binadamu kuna umajimaji unaofyonzwa kutoka nje ya ubongo kila baada ya saa 8.

Lakini kwa Guto, maji hayo hayakufyonzwa na mkusanyiko wa maji maji hayo uliweka shinikizo kwenye eneo hilo, na kusababisha maumivu mengi.

Kwa Guto, jambo gumu zaidi kukumbana nalo katika hali hii lilikuja baada ya upasuaji, na kutengwa. "Walinifungia kwenye chumba cha vioo ili wanichunguze kwa ujumla ili kuona kama sitakuwa na kifafa, ikiwa nitaweza kuongea, kuona na kusogeza miguu yangu," anakumbuka kijana huyo.

Mwishoni mwa uchunguzi huo mgumu wa kimatibabu, ilibainika kila kitu kilikuwa sawa. Hata hivyo, kuondolewa kwa uvimbe huo kuliathiri tezi ya muhimu ya pituitary ambayo iko sehemu ya chini ya ubongo- hufanya kazi ya kuzalisha homoni ya ukuaji miongoni mwa kazi nyingine.

"Walinifanyia vipimo vingi na kubaini kwamba nitaacha kukua, lakini hawakujua ni lini haswa. Ningeweza kuacha kukua nikiwa na miaka 8, 9 au 10. Mwishowe niliacha kukua nikiwa na miaka 12," anaeleza kijana huyo.

Uvimbe wa ukubwa wa maharagwe

Madaktari waliondoa 20% ya uvimbe huo ili kuepuka kuathiri maeneo mengine ya ubongo. Lakini baadaye walilazimika kumfanyia upasuaji mwingene mara mbili.

"Katika upasuaji wa kwanza, mrija uliwekwa ili kuondo umajimaji kutoka kwa ubongo hadi kwenye tumbo (inayoitwa ventriculoperitoneal shunt, au PVD); na katika upasuaji wa pili, mrija uliwekwa ndani ya uvimbe na kwenda hadi hifadhi ya kichwa chini ya ngozi, ili kufanyiwa tiba ya mionzi inayofahamika kama chemotherapy," anaelezea daktari wa upasuaji wa neva aliyemfanyia upasuaji huo, Nério Azambuja Jr.

Guto alikuwa na wakati mgumu kukubali mwonekano wake

Chanzo cha picha, PERSONAL FILE

Maelezo ya picha, Guto alikuwa na wakati mgumu kukubali mwonekano wake, lakini kwa miaka mingi ameweza kuishi maisha ya utulivu kutokana na upendo wa familia yake.

Kulingana na Guto, tiba ya chemotherapy ilichukuwa muda mrefu na athari yake ilikuwa ilikuwa kaubwa. “Mwanzoni niliifanya mara tatu kwa wiki, ikashuka hadi mbili, mara moja kwa mwezi, mpaka ikaisha, lakini niliteseka sana, kwa sababu mrija niliyowekewa ilikuwa inauma sana, kanda na hilo walinichoma sindano kubwa ndani ta mrija huo, hebu tafakari. ,” anasema kijana huyo. .

Wakati huo, kulikuwa na uwezekano wa kushawishi ukuaji wa homoni, lakini uwezekano kwamba uvimbe pia kukua wakati huo huo ulikuwa juu, kwa hiyo aliamua kutofuata chaguo hilo.

Katika ujana, alipogundua kuwa sura yake haibadiliki tena, kwamba alikuwa amedumaa, Guto alikabiliwa na kibarua kingine kigumu: cha kukubalika muonekano wake.

“Nilipokuwa na umri wa miaka 15 hivi, niliishia kuwa mkaidi, sikuzungumza na mtu, sikutoka darasani kwenda mapumziko, sikumjibu mwalimu ambaye alikuwa na tabia kumpigia simu shangazi yangu," anakumbuka.

Hata hivyo kadiri muda ulivyosonga, Guto alikubali zaidi sura yake ya ujana na, kutokana na upendo aliyoonyeshwa na familia yake, leo anaishi maisha ya utulivu akiwa na shangazi na binamu yake.

"Bila familia yangu, nisingeweza kukabiliana na hali hii," anasema.

"Leo hii sijali watu wanasema nini kuhusiana na mwonekano wangu, nina marafiki wadogo kwa wakubwa, wenye umri wa miaka 20, 30, 40, na hawanihukumu, hawasemi chochote kunihusu. Kila mtu hapa ananijua. , wananipigia simu kuninunulia simu, runinga Na leo niko vizuri sana, naongea sana na sioni aibu kwa lolote,” anasema kijana huyo mwenye ndoto ya kuwa mpiga picha na ana matumaini ya kununua kamera ya kitaalamu hivi karibuni.

Kwa jumla, alipokea matibabu kwa miaka 15, iliyojumuisha tiba saba ya chemotherapy na upasuaji wa kichwa mara 12. Hata hivyo, uvombe haikuondolewa wate kwa asilimia 100.

Guto aliacha kupokea chemotherapy mnamo 2015 na ameishi na uvimbe wa ukbwa wa maharagwe na haumwa natena na kichwa tangu wakati huo.