Njia nne anazotumia Zelensky kuelekeza ulimwengu kwenye mzozo wa Ukraine

Iliyochapishwa

Huku majeshi yakiwa mstari wa mbele kukabiliana na uvamizi wa Urusi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekuwa akiendeleza kampeni ya kuhakikisha msaada wa kimataifa kwa nchi yake haitafifia.

Ili kufanikisha hili Bw. Zelensky amekuwa akiendesha shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na kukutana na mlolongo mrefu wa viongozi wa kimataifa mjini Kyiv, kupiga picha na watu mashuhuri na hata kuonekana kwenye hafla za kiteknolojia.

Kwa kuwa inakabiliana na nchi iliyo na uwezo mkubwa wa kijeshi, Ukraine inahitaji jamii ya kimataifa kuisaida kuzuia vikosi vya Urusi kusonga mbele.

Kupata uungwaji mkono huu, kundi la maafisa wa uhusiano mwema wa rais limepata njia za bora zaidi ya kuelekeza ulimwengu kwenye madhila inayopitiwa na nchi yake.

Kuomba msaada kupitia Hologram

Wiki iliyopita, Bw Zelensky aliangazia "Star War" alipozungumza na viongozi wa kiteknolojia kupitia hologram wakati wa kongamano la VivaTech mjini Paris.

"Sio jambo la kawaida kwa raids ama wakuu wa serikali kutumia hologram kuwahutubia watu," Bw. Zelensky alisema.

"Lakini hii haikuwa wakati pekee wa 'Star Wars' ambayo tunayatekeleza kwa vitendo. Tutashinda Dola pia," aliongeza, akilinganisha vikosi vya Kirusi na watu wabaya katika franchise maarufu ya filamu duniani.

Madhumuni ya hotuba hiyo ilikuwa kuyapa makampuni ya teknolojia "nafasi ya kipekee" kuingia katika ujenzi wa nchi na kuunda "demokrasia kamili ya kidijitali" nchini Ukraine.

'Ushawishi wa watu maarufu'

Uhamasishaji wa umma kuhusu mzozo huo umeimarishwa na idadi kubwa ya watu mashuhuri zaidi duniani ambao, tangu mwanzo wa vita, waliunga mkono Ukraine na kuchangisha mamilioni ya kusaidia wakimbizi.

Watu hao mashuhuri ni pamoja na mwanasoka wa zamani David Beckham, mwanamuziki Ed Sheeran, na waigizaji Sean Penn, Ashton Kutcher na Mila Kunis - ambaye ni raia wa Ukraine.

Mwigizaji Angelina Jolie, ambaye ni mjumbe maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) alitembelea Ukraine mwezi Aprili ambapo alikutana na wafanyakazi wa kujitolea na wakimbizi.

Bw Zelensky ambaye pia alikuwa mchekeshaji maarufu kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Ukraine si mgeni katika masuala ya uhamasishaji, amechanganyaka vyema na waigizaji wake wanaomuunga mkono.

Siku ya Jumatatu alimkaribisha muigizaji Ben Stiller mjini Kyiv kama sehemu ya ziara ya Stiller katika eneo hilo Siku ya Wakimbizi Duniani - Muigizaji huyo mashuhuri pia ni balozi wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa.

"Ni heshima kubwa kwangu. Wewe ni shujaa wangu," nyota huyo wa Hollywood alimwambia rais.

Mwanzoni mwa mwaka, Mtangazaji wa Oscar Amy Schumer alisema ametoa ombi la kumpata Bw. Zelensky kuhutubia waigizaji nyota wa Hollywood kupitia mtandao wa Skype wakati wa hafla hiyo "kwasababu tuzo hiyo huvutia watu wengi duniani".

Kuwakaribisha wanasiasa (au kuwa mgeni wa kawaida)

Picha kama hizo zinafanyika sambamba na juhudi za kuwashawishi viongozi wa Muungano wa Ulaya kukubali kutoa hadhi ya mgombea ya Ukraine kujiunga na muungano huo, pamoja na maombi ya silaha zaidi.

Miongoni mwa wakuu wa nchi ambao wametembelea Kyiv siku za hivi karibuni ni Rais Emmanuel Macron (Ufaransa), Mario Draghi (Italia), Olaf Scholz (Ujerumani) na Klaus Iohannis (Romania).

Orodha hiyo ndefu pia inajumuisha Boris Johnson wa Uingereza na Justin Trudeau wa Kanada, lakini isipokuwa Joe Biden.

Rais wa Marekani amepata mabilioni ya dola na silaha kwa ajili ya Ukraine lakini amesema hataki "kusababisha ugumu zaidi kwa Waukraine" kwa kuongeza nafasi ya mahali atakapozu katika safari yake ijayo ya Ulaya.

Mataifa yasiyo ya Magharibi yamegawanyika zaidi katika uungaji mkono wao kwa Ukraine katika vita hivyo, ingawa Bw Zelensky amekuwa akitafuta uungwaji mkono wao, akitoa tahadhari kwa matokeo mabaya ya vita hivyo kwa mataifa mengine duniani katika hotuba yake kwa Umoja wa Afrika (AU). Jumatatu.

Alisema Waafrika wamekuwa "mateka" wa vita hivyo na wanakabiliwa na hatari ya njaa kwa sababu vita hivyo vimesababisha uhaba wa nafaka na mbolea - lakini BBC imebaini kuwa ni viongozi wanne tu wa Kiafrika kati ya 55 walioalikwa waliohudhuria wito huo.

Mikutano mingine ya video imehudhuriwa vyema zaidi, hata hivyo, na Zelensky amepongezwa kwa hotuba alizotoa kwa Bunge la Marekani na mabunge ya EU, Ujerumani, Japan, Ufaransa, Uhispania na Italia, miongoni mwa mabunge mengine.

Kuonesha ulimwengu

Bw. Zelensky pia amefanya kila awezalo kuonesha ulimwengu uharibifu mbaya uliosababishwa na vita nchini mwake, akizuru miji iliyobomolewa na kuwatembelea wanajeshi vitani na katika hospitali.

Alifanya ziara yake ya kwanza katika eneo la kusini mwa Ukraine Jumamosi iliyopita na kwenda hadi mji wa Mykolaiv.

Wakayi wa ziara hiyo, Bw. Zelensky alikagua majengo yaliyoharibiwa na kukutana na maaskari, maafisa na wahudumu wa afya.

Kiongozi huyo wa Ukraine pia alizuru mji wa magharibi wa Odesa, ambao umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na makombora ya Urusi tangu mwanzo wa vita.

Katika wiki za hivi karibuni Rais amezuru miji mingine ambayo inakabiliwa na mapigano, ikiwa ni pamoja na Kharkiv upande wa mashariki,akikaidi majeshi ya Urusi kwa kwenda maeneo ambapo mapigano yamekuwa yakiendelea.

'Usigeukie kitu kingine'

Wakati wanajeshi wa Ukraine wakipambana vitani, rais ameonyesha dhamira ya kuhakikisha ulimwengu huelekezi macho kutoka kwa Ukraine katika wakati huu mgumu.

Amejihusisha na hadhira mbalimbali zinazojumuisha watu mashuhuri na viongozi wa dunia, wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani na vyombo vya habari vya kimataifa, pamoja na makusanyo ya viongozi wa biashara kutoka Doha hadi Davos.

Mwezi uliopita, hata alichukua Tamasha la Filamu la Cannes kwa mshangao, akitoa anwani isiyopangwa kwenye sherehe ya ufunguzi na kupokea pongezi. Siku ya Jumatatu aligusia kiini cha kampeni yake ya kuwafikia watu wakati akirejea Cannes (karibu), kwa kufungua tamasha la Simba la Ubunifu.

"Hata wakati wa vita, una uwezo wa kufikia kina cha roho ya mwanadamu," aliiambia hadhira ya wabunifu.

"Unafanya kila mtu azungumzie hili suala kila siku la sivyo litasahaulika," alisema, kabla ya kuto awito wake.

"Zungumzieni Ukraine," Bw. Zelensky alisema. "Msikubali ulimwengu ugeuie kitu kingine chochote."