Vifaa vingine vya mawasiliano vyaripotiwa kulipuka Lebanon

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Shirika la Habari la Kitaifa la Lebanon (NNA) linaripoti kuwa watu tisa wamefariki na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa baada ya "vifaa" kudaiwa kulipuka katika mji wa Sohmar, kusini mwa Bonde la Bekaa.

Milipuko ya hivi punde pia inahusisha vifaa vya mawasiliano vinavyotumiwa na Hezbollah, chanzo cha usalama kililiambia shirika la habari la Reuters.

Idadi kubwa ya waliojeruhiwa wameumia sehemu ya tumbo na mikono, chanzo kiliongeza.

Hali ya taharuki imeendelea kushuhudiwa katika kitongoji cha Dahiya, kusini mwa mji wa Beirut na ngome ya Hezbollah.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa milipuko inatokea kote nchini humo, kila mtu anashuku watu wanaotumia simu au vifaa vingine.