Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tazama: Jinsi magari yalivyotumbukia mtoni baada ya daraja kuharibiwa na kimbunga
- Author, Kelly Ng
- Nafasi, BBC News
- Author, Christy Cooney
- Nafasi, BBC News
- Iliyochapishwa
- Muda wa kusoma: Dakika 1
Daraja lenye shughuli nyingi kaskazini mwa Vietnam liliporomoka baada ya kukumbwa na kimbunga kiitwacho Super Typhoon Yagi, ambacho kimeua zaidi ya watu 60 tangu kilipotua siku ya Jumamosi.
Picha za kamera ya ndani ya gari zilionyesha wakati daraja la Phong Chau katika mkoa wa Phu Tho lilipoporomoka Jumatatu, na kutumbukiza magari kadhaa kwenye maji . Utafutaji ulikuwa ukiendelea kwa watu 13 waliozama.
Kimbunga chenye nguvu zaidi nchini Vietnam katika kipindi cha miaka 30 kimesababisha maafa kote kaskazini mwa nchi hiyo, na kuwaacha watu milioni 1.5 bila umeme.
Ingawa sasa nguvu yake imedhoofika katika hali ya unyogovu wa kitropiki, mamlaka imeonya Yagi italeta usumbufu zaidi inapoelekea magharibi.