Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 19.04.2024
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Jamal Musiala anaibuka kama shabaha kuu ya Manchester City msimu wa joto, huku Chelsea pia wakifuatilia hali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Guardian)
Hata hivyo, Bayern hawana nia ya kumuuza Musiala na wanatayarisha ofa ya mkataba mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Fabrizio Romano)
Arsenal wanatazamia kumsajili mshambuliaji na winga katika msimu wa joto, huku mshambuliaji wa Newcastle Uswidi Alexander Isak, 24, na winga wa Ufaransa Michael Olise, 22, ambaye yuko Crystal Palace, wakiwa miongoni mwa malengo yao. (Guardian)
Arsenal inamfuatilia mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 20 huku wakiongeza juhudi za kusajili mshambuliaji msimu huu. (Standard)
Chelsea na Manchester United pia wanamfuatilia Sesko, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro milioni 50. (Ben Jacobs)
Meneja msaidizi wa Liverpool Pep Lijnders ananyatiwa na Besiktas kwa ajili ya nafasi ya kocha mkuu wa timu hiyo ya Uturuki iliyo wazi. (Athletic- Usajili unahitajika)
Liverpool na Paris St-Germain wanafikiria kumnunua mlinzi wa Chelsea na Uingereza Levi Colwill, 21. (GiveMeSport)
Tottenham wanavutiwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry, huku Bayern Munich wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 28. (Football Insider)
Spurs pia wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa Nottingham Forest Morgan Gibbs-White, 24, na wako tayari kumnunua Muingereza huyo msimu wa joto. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku anatarajiwa kurejea Chelsea mwishoni mwa msimu wake wa mkopo wa muda mrefu nchini Italia huko Roma, ambayo haiweza kumudu euro milioni 43 kumsajili mchezaji huyo wa miaka 30 kwa mkataba wa kudumu. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Chelsea na Newcastle United wanavutiwa na mlinda lango wa Arsenal na Uingereza Aaron Ramsdale, 25. (CaughtOffside)
Mkufunzi wa Ujerumani Julian Nagelsmann haongei tu na Bayern Munich kuhusu kuwa meneja wao na atafanya uamuzi ndani ya wiki ijayo au zaidi, kulingana na wakala wake. (Podikasti ya Spielmacher, kupitia Metro)
Kocha wa zamani wa Liverpool na Everton Rafael Benitez anatazamiwa kuinoa Sao Paulo mwezi mmoja baada ya kutimuliwa na Celta Vigo. (Sun)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi