Kuibuka na kuongezeka kwa muziki wa chuki dhidi ya Uislamu nchini India 

ggg
Maelezo ya picha, Chaturvedi alianza kazi yake kama mwimbaji wa nyimbo za ibada
Iliyochapishwa

Sandeep Chaturvedi, 26, anajiandaa kurekodi wimbo wake mpya katika studio ya muda kwenye jiji la Ayodhya katika jimbo la kaskazini mwa India la Uttar Pradesh. 

Wimbo huo unahusu msikiti mmoja ambao umezua utata baada ya Wahindu kudai kuwa na haki ya kuabudu humo. Imejawa na minong'ono dhidi ya Waislamu. 

Lakini Chaturvedi anasema wimbo huo unaweza kumrudisha vizuri katika biashara ya muziki. 

Nyimbo za Chaturvedi ni sehemu ya mtindo unaokua wa muziki kwenye YouTube na majukwaa mengine ya mitandao ya kijamii ambapo wafuasi wa mrengo wa kulia wa Kihindu wanawamiminia sumu Waislamu. 

Nyimbo hizo ni za matusi na wakati mwingine za kutisha. Kawaida zinatokana na dhana kwamba Wahindu wameteseka kwa karne nyingi mikononi mwa Waislamu na sasa ni wakati wa malipo. 

Mwandishi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa Nilanjan Mukhopadhyay anasema pamoja na kuwa chanzo cha mapato, muziki huo huwavutia waimbaji wao. Lakini kwake, huu sio muziki. "Hiki ni kilio cha vita. Ni kana kwamba muziki unatumiwa kushinda vita. Haya ni matumizi mabaya ya muziki na hii imekuwa ikitokea kwa miaka mingi sasa." 

ggg
Maelezo ya picha, Chaturvedi anarekodi nyimbo zake studio

Chaturvedi alianza kazi yake kama mwimbaji wa nyimbo za kidini takriban muongo mmoja uliopita, lakini alibadilika miaka michache baadaye alipoamua kutunga nyimbo kuhusu "Uhindu na utaifa". Wazo, anasema, lilikuwa kupata uboreshaji wa hali halisi ya mambo. 

Alifanya vizuri sana wakati video ya muziki aliyotayarisha mwaka wa 2016 ilipovuma mara moja miongoni mwa mfumo wa ikolojia wa Kihindu wa mrengo wa kulia. 

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mashairi ya haya hayawezi kutolewa tena hapa. Lakini sauti ya wimbo huo ilikuwa ya moja kwa moja: onyo kwa jamii ya Waislamu kuhusu kitakachotokea siku utaifa wa Kihindu utakapoinuka. 

Chaturvedi anasema wimbo huu ulipata maoni ya mamilioni kwenye YouTube kabla ya kituo chake kusimamishwa, kufuatia maelfu ya malalamiko. Anawalaumu Waislamu kwa kuripoti wimbo wake kama maudhui yasiyofaa. 

Anaogopa kupoteza "mamilioni ya waliojisajili", lakini anakataa kufichua pesa alizokuwa akipata kutoka YouTube. Alisema inamgharimu takriban rupia 20,000 (£207; $253) kuunda video ya muziki. 

"Sikuwa nikipata pesa nyingi kutoka YouTube. Kilicho muhimu zaidi ni kutambuliwa kwangu kama mwimbaji mwanamapinduzi wa kitaifa," anasisitiza. 

Chaturvedi ameunda kituo kipya kwenye YouTube tangu wakati huo. Lakini idadi ya maoni kwenye baadhi ya maudhui aliyopakia sio ya kutia moyo. Anatarajia kubadilisha hilo katika wimbo wake mpya. 

Mara nyingi amekua akishutumiwa kuwalenga Waislamu kupitia muziki wake, Chaturvedi hajawahi kuomba msamaha. "Nikikusihi kwa kukunja mikono ili nipate kilicho changu, utakubali? Hutaweza. Kwa hiyo inabidi tufanye uchochezi, sivyo?" 

Upendra Rana ni mtayarishaji mwingine anayetengeneza muziki kama huo huko Dadri karibu na Delhi. 

Dhamira yake ni "kusahihisha" historia na nyimbo zake zinawasifu watu wa jamii ya Kihindu ambapo watawala wa Kiislamu wanaonyeshwa kama wabaya. 

“Mambo mengi ambayo ni ya kweli yamefichwa huku uongo ukiwekwa kwetu,” anadai alipokuwa akizungumzia historia inayofundishwa shuleni. 

ggg
Maelezo ya picha, Upendra Rana ana mamia ya maelfu ya waliojisajili kwenye chaneli yake ya YouTube

Rana anasema kwamba anapata mapato ya kutosha kutokana na video anazopakia kwenye YouTube. 

"Tunaingiza fedha za kigeni nchini India. YouTube inalipa kwa dola," anaashiria, akionyesha Kitufe cha Kucheza cha Silver cha YouTube kilichowekwa ukutani ambacho kinashiriki nafasi na picha za wapiganaji wa Kihindu. 

Tangu Rana alipohama kutoka kutunga nyimbo za kidini na mapenzi hadi zile zenye sauti za "kihistoria", amekuwa aina ya nyota katika eneo la Dadri. Ana karibu wafuasi 400,000 katika akaunti yake ya YouTube na nyimbo zake nyingi zimetazamwa na mamilioni ya watu. 

Rana anasema kutengeneza video ya muziki kunamgharimu rupia 8,000 tu (£84; $100). Ana studio yake ya kurekodi na kuhariri video na timu inayojumuisha mtu anayerekodi video sambamba na mhariri. 

Bw Mukhopadhyay anasema mtindo wa kurekodi muziki kama silaha dhidi ya walio wachache unakumbusha matukio yaliyowahi kutokea siku za nyuma. Anakumbuka mpango wenye utata wa uwekaji mawe wa msingi huko Ayodhya mwaka wa 1989 ulioandaliwa na shirika la mrengo wa kulia la Vishwa Hindu Parishad (VHP) ambao uliishia kwa kubomolewa kwa msikiti wa Babri mnamo 1992. 

"Hapo awali, tasnia ya kanda za sauti ilikuwa ikifanya vizuri. Zilikuwa na nyimbo za kidini na kile kinachoitwa kauli mbiu za uchochezi zinazohusiana na suala la Ram Janmabhoomi [Wahindu wanaamini kwamba Ayodhya ni mahali pa kuzaliwa kwa Bwana Ram] na kanda hizi zilikuwa zikichezwa kwenye maandamano kuhamasisha watu." 

Miongo mitatu baadae , imesambaa sana. 

Nyimbo zinazotangaza "ikiwa unataka kuishi India, jifunze kusema Vande Mataram ("Nakusifu, Mama") ..na jifunze kuishi ndani ya mipaka yako", au "kuwaza Wahindu kama watu dhaifu ni kosa la adui" hafanyi juhudi zozote za kuficha yule wanayemlenga. 

Nyimbo hizi pia zimesaidia mashirika ya mrengo wa kulia "kuhamasisha" wafuasi wao. 

ggg
Maelezo ya picha, Nyimbo hizi za "kizalendo" hutazamwa na vijana wengi

"Vijana hupenda nyimbo hizi wanapoongeza shauku na ari yao," anasema Pinky Chaudhary, ambaye anaongoza kundi la mrengo wa kulia la Hindu Raksha Dal. Anasema kuwa nyimbo hizo husaidia kujenga ufahamu miongoni mwa vijana. 

"Ninahisi msukumo wa ghafla na nguvu ninaposikiliza nyimbo hizi. Zinanikumbusha mambo ambayo tulifanyiwa wakati fulani na ambapo tumefikia sasa," anasema Vijay Yadav. 

Msanii wa michoro anayeendelea na masomo yake kutoka Lalit Kala Akademi, chuo cha kitaifa cha sanaa ya urembo cha India, Bw Yadav, 23, anasema anapenda kusikiliza aina hii ya muziki. 

Mazungumzo haya ambayo Yadav anazungumzia yaliaminika kuonyeshwa Aprili mwaka huu kipindi cmbacho mapigano makali yaliporipotiwa kutoka majimbo kadhaa wakati wa sherehe za Kihindu. 

ggg
Maelezo ya picha, Rana ana sehemu yake ya kurekodi na kuhariri video

Wakati wa matukio haya, muziki wa kukera ulisikika kupitia vipaza sauti wakati Wahindu waliofanya maandamano ya kidini na kuhamia karibu na maeneo yenye Waislam wengi. 

Katika baadhi ya makabiliano haya, nyimbo za uchochezi ikiwa ni pamoja na utunzi wa Chaturvedi wa mwaka 2016, zilidaiwa kuchangia pakubwa katika kuongeza ghasia hizo. 

Hata hivyo Chaturvedi anakanusha madai hayo. 

"Ninajaribu tu kujenga ufahamu kupitia muziki wangu. Hakuna kinachotoka kwa upendo. Tunapaswa kupigana na kunyakua kile ambacho ni chetu."