Ndani ya 'chumba cha kudhibiti vita' cha jeshi la Israeli kwenye mpaka na Lebanon
Na Anna Foster
BBC News, Israel ya Kaskazini

Chanzo cha picha, IDP
Wanakiita "Hamal" - kifupi cha "chumba cha vita" kwa Kiebrania. Kiko juu ya milima kwenye mpaka wa Israel-Lebanon, katikati mwa eneo lililolindwa na kuta zisizoweza kulipuliwa na mlipuko.
Kila kitu hapa ni kuhusu usalama. Hakuna madirisha, na kabla ya kupita kwenye mlango thabiti inabidi uache simu za mkononi na saa za smart- chochote ambacho kinaweza kutoa kufichua siri ya ni wapi eneo hili lilipo.
Ndani ni vyumba vya wachunguzi, muda wote , kikosi cha askari kinawatazama kwa makini.
Kila moja inaonyesha picha za rangi nyeusi-na-nyeupe kutoka kwa kamera ambazo huongozwa kila mara zilizopo kwenye zaidi ya kilomita 100 (maili 62) kutoka kwenye mpaka wa Lebanon.
Mabadiliko kwa kawaida huchukua muda wa saa nne, kutazama mzunguko wa picha mara kwa mara na kutafuta kitu chochote kisicho cha kawaida.
Tangu wanamgambo wa Hamas wa Palestina waliposhambulia kusini mwa Israel kutoka Gaza siku 11 zilizopita, na kuua watu 1,400 na kuwachukua mateka wengine 199, kumekuwa na ongezeko la hali ya wasi wasi katika mpaka huu.
Takriban kila siku wanamgambo wa Hezbollah kutoka Lebanon wanarusha makombora ya vifaru hadi Israel, na vikosi vya Israel vimejibu kwa mizinga, ndege za kivita na helikopta za mashambulizi.
Pande zote mbili zimeshuhudia vifo vya raia wiki hii. Kila malumbano yanazua hofu kwamba ghasia kwenye mpaka huu zinaweza kushindwa kudhibitiwa.

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kapteni "S" ndiye anayeiongoza kampuni hii ya wanawake pekee kuangalia kamera. Kazi hii ya ufuatiliaji inafanywa na wanawake pekee.
"Sisi ni macho ya askari, macho ya vikosi katika uwanja - wa mpaka mzima." ananiambia, "na tuna jukumu muhimu sana."
Upande mmoja wa chumba, picha za utotoni za kila mwanajeshi zimebandikwa ukutani.
Tarehe zao za kuzaliwa zimeandikwa kwa kalamu ya wino uliokolezwa kwa wino mweusi. Kila mmoja ni kijana, wengi wao bado wanamaliza muda wao wa huduma ya kijeshi ya lazima katika Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF).
"Sisi ni wanawake wenye nguvu, askari wa kike ambao wanajua kazi na jukumu lao na tunajua kuwa tuna jukumu muhimu sana katika vita hivi.
"Lengo letu kwanza ni kulinda, na wasichana wote wanajua. Kila askari anakuja kwa zamu yake akiwa macho na anajua sehemu yake."
Mara kadhaa katika wiki iliyopita, wanamgambo wamejaribu kuvuka ukuta.
Kundi lenye nguvu la kijeshi na kisiasa la Lebanon la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran, hatua kwa hatua limeongeza juhudi zake za kujipenyeza ndani ya Israel.
Kama mshirika wake mkuu Hamas, imetangazwa kuwa shirika la kigaidi na Marekani, Uingereza na wengine.

Kuna wasiwasi wa kweli kimataifa kwamba upotoshaji wowote hapa unaweza kusababisha kufunguliwa kwa awamu mpya ya kaskazini katika vita hivi. Tukio kubwa - kama mlipuko wa hospitali huko Gaza, au kuanza kwa mashambulizi ya ardhini huko na Israeli - pia inaweza kusababisha Hezbollah kuchukua hatua muhimu zaidi kwa Israeli.
Nyakati fulani, unahisi ukaribu sana wa vita. Sajenti "I" alikuwa kazini, akitazama mtambo wake wa ufuatiliaji wa vita wakati picha zake zilibadilika ghafla.
Kivuli cha watu kilipokaribia ukuta wa mpaka, alijua la kufanya. Haraka, aliagiza shambulio la anga.
"Nilitambua kundi la magaidi kwenye skrini na nikaelewa kuwa kuna kitu kibaya. Hii ni kazi yangu, kulinda mpaka wa kaskazini ili mtu yeyote asipenye na hakuna raia atakayeumia, haswa wanaoishi hapa mpakani."
"Inatisha, na inatia msongo wa mawazo, lakini lazima nitulie, sitasema uongo, inatisha sana kusimama hapa mpakani. Kwa yote yanayotokea siku hizi katika nchi yetu, ni vigumu sana kushughulikia yote yaliyotokea. "
Kwa Sajenti "I", ni ngumu sana. Wanajeshi vijana wa kike wanaofanya kazi sawa na yao kusini walilengwa na Hamas.
"Nafikiria vikosi vyote na waangalizi wa kamera waliokwama kwenye shambulizi huko. Moyo wangu unawasikitikia. Mimi binafsi ninafahamu watu wengi waliotekwa nyara au kuuawa."














