Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 01.05.2024
Manchester United haitarajii klabu yoyote kufikia thamani ya £70m ya mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 26, msimu huu wa joto. (ESPN)
Paris St-Germain wamepiga breki nia yao ya kutaka kumnunua Rashford na watafuatilia malengo mengine ya uhamisho kabla ya dirisha la kiangazi. (i Sport)
Wakati huo huo, kocha wa United Erik ten Hag, 54, hajui kama atakuwa kocha wa Old Trafford msimu ujao. (HITC)
Arsenal wamempa kiungo wa Italia Jorginho mkataba mpya na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anatarajiwa kuusaini. (Athletic- Usajili unahitajika)
West Ham itakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan kumnunua kocha wa Lille Paulo Fonseca huku mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 51 akionekana kuchukua nafasi David Moyes wa Hammers. (i Sports)
Moyes, 61, anawaniwa na Spartak Moscow huku kukiwa na suitafahamu juu ya mustakabali wake katika klabu ya West Ham. (Mail)
Mshambulizi wa Chelsea na England Raheem Sterling, 29, hajawasiliana na Ligi ya Saudi Pro kuhusu uhamisho wa majira ya kiangazi, hata hivyo, The Blues watakuwa tayari kumuuza mshambuliaji wa Ubelgiji kwa mkopo Romelu Lukaku, 30, kwao. (Caughtoffside)
Kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 29, amedokeza kuwa atafikiria mustakabali wake Manchester United baada ya Euro 2024, lakini kwa sasa anaangazia fainali ya Kombe la FA na dimba nchini Ujerumani msimu huu wa joto. (Danz Ureno - kwa Kireno)
Vilabu kadhaa nchini Saudi Arabia vinavutiwa na mshambuliaji wa Barcelona mwenye umri wa miaka 21 Ansu Fati, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Brighton, na mlinzi wa zamani wa Ufaransa Clement Lenglet, 28, ambaye yuko Aston Villa kwa mkopo . (Sport - kwa Kihispania)
Manchester United bado wanapanga kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22, msimu huu wa joto, na uamuzi wa mwisho kufanywa mwishoni mwa msimu. (Fabrizio Romano)
Chelsea wamekanusha kuwa walilipia ndege ya Ruben Amorim kuelekea London wiki iliyopita, au kwamba walikuwa na mikutano yoyote na bosi huyo wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 39. (Matt Law, Telegraph, kupitia X)
Borussia Dortmund wanataka kumbakisha Ian Maatsen katika klabu hiyo zaidi ya msimu huu kufuatia winga huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 22 kufanikiwa kwa mkopo kutoka Chelsea. (Fabrizio Romano)
Leicester wamefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Uingereza Jamie Vardy mwenye umri wa miaka 37 kuhusu kuongeza muda wake wa kusalia katika klabu hiyo. (Mail)
Crystal Palace huenda wakamuuza kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Killian Phillips, 22, katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Team Talk)
Kiungo wa kati wa Uingereza Callum O'Hare, 25, ambaye anawaniwa na Aston Villa na West Ham, ameiambia Coventry City kuwa ataondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bure msimu huu wamajira ya joto. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi