Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 27.06.2022

TH
Iliyochapishwa

Mlinda mlango wa Marekani Matt Turner anasema "ameweza kutimiza ndoto yake" baada ya kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Arsenal.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na The Gunners kwa mkataba wa muda mrefu - ambao ulikubaliwa mwezi Februari - kutoka klabu ya  MLS New England Revolution.

Alicheza mechi 102 akiwa na New England katika kipindi cha miaka sita akiwa na klabu hiyo.

"Nilipotazama Arsenal nikiwa mtoto, nilipenda jinsi timu inavyocheza na maadili ya klabu hii," Turner alisema.

Mnamo 2020, Turner alitajwa kuwa mchezaji wa thamani zaidi kwa mashabiki na wachezaji wenzake huko New England na, mnamo Agosti 2021, aliwakilisha MLS kwenye Mchezo wa Nyota wa MLS ambapo aliokoa penalti mbili. 

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambulizi wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus, 25, amekubali mkataba wa miaka mitano na Arsenal. (Guardian)

Liverpool wana uhakika wa kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham(Sun)

West Ham wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse, 27, msimu huu wa joto. (Sky Sports)

Mchezaji wa Denmark Christian Eriksen anakaribia kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake, huku Tottenham sasa wakiangalia walengwa wengine lakini Brentford wana matumaini ya kumnunua tena mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Fabrizio Romano)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Ajenti wa Sadio Mane amemkana fowadi huyo wa Senegal, 30, aliondoka Liverpool na kujiunga na Bayern Munich msimu huu wa joto kwa sababu hakuwa anapokea pesa za kutosha Anfield. (TVMondo, via Mirror)

Villarreal na West Ham wamefanya mazungumzo juu ya winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma, 25. (Toni Juanmarti - in Spanish)

Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anaweza kuwa na pauni milioni 100 tu kuijenga upya klabu hiyo msimu huu wa joto. (Sun)

Tottenham wameulizia kuhusu beki wa RB Leipzig wa Croatia Josko Gvardiol, 20. (Nabil Djellit - in French)

 

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Angel di Maria, ambaye mkataba wake na Paris St-Germain unamalizika mwishoni mwa Juni, anakaribia kuhamia Juventus, licha ya Barcelona kusalia kwenye picha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 34. (Calciomercato - in Italian)

Beki wa Manchester United Brandon Williams, 21, hana mahitaji ya ziada Old Trafford na anaweza kupatikana kwa £10m msimu huu wa joto. (Mail)

Atletico Madrid wanamfuatilia beki wa Celtic wa Croatia Josip Juranovic, 26. (Record)

Monaco inamwinda mshambuliaji wa Torino na Italia Andrea Belotti, 28, huku AC Milan pia wakiwa mbioni kumsajili. (Ekrem Konur)

Leeds wamewatambua kiungo wa RB Leipzig na Marekani Tyler Adams, 23, na kiungo wa kati wa RB Salzburg kutoka Mali Mohamed Camara, 22, kama mbadala wa nyota wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, ambaye anaonekana kukaribia Manchester City. (Mail)

Mshambulizi wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo, 37, amekataa nafasi ya kujiunga na Inter Miami ya David Beckham na atasalia Old Trafford. (Star)