Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 31.05.2024
Manchester United wanafikiria kumnunua beki wa Chelsea Muingereza Trevoh Chalobah, 24. (Independent)
Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Colombia, Luis Diaz na mlinzi wa Uingereza Joe Gomez, wote 27, wanawaniwa na klabu za ligi ya Saudi Pro huku zinatazamia kuwapata wachezaji wachanga msimu huu. (Mail)
Tottenham inapokea ofa ya kuwauza wachezaji wa kimataifa wa Brazil. Wazezaji hao ni mshambuliaji Richarlison, 27, na beki Emerson Royal mwenye umri wa miaka 25. (Standard)
Mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 20, anapendelea kuhamia Arsenal msimu huu wa joto. (Mirror)
Arsenal wako tayari kuendelea na mpango wao wa kumnunua Sesko kwa pauni milioni 55. (HITC)
Everton wameiambia Manchester United kusahau mpango wa kumsajili beki wa England wa chini ya umri wa miaka 21, Jarrad Branthwaite kwa bei nafuu. The Toffees wanataka mara mbili ya £40m inayopendekezwa na United . (Mirror)
Manchester United wanafikiria kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood zaidi ya mwaka ujao ili kuhakikisha mauzo ya kudumu yanakamilika. Juventus, Napoli, Atletico Madrid na Borussia Dortmund pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (i Sport)
Atletico Madrid wanaibuka kidedea kuwania saini ya Greenwood. (HITC)
West Ham wako kwenye mazungumzo na Palmeiras kuhusu kumnunua kiungo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 18 Luis Guilherme. (Fabrizio Romano)
Arsenal wanajiandaa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua beki wa kushoto wa Uholanzi Quilindschy Hartman, 22, kutoka Feyenoord. (Telegraph - usajili unahitajika)
Monaco wako mbele zaidi kuliko Watford au AC Milan katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Crystal Palace wanajadiliana na Sunderland kuhusu mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Jobe Bellingham, 18, ambaye pia anaweza kucheza katika safu ya kiungo. (Standard)
Brentford pia wanavutiwa na Bellingham. (Athletic - usajili unahitajika)
Everton wameonesha nia ya kutaka kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Ross Barkley, 30, kutoka Luton Town lakini wanatazamiwa kushindwa na Aston Villa. (Football Insider)
Manchester United wanajadiliana na kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 18, kuhusu kusaini kandarasi mpya katika klabu hiyo. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi