Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 13.06.2024
Beki wa Liverpool na England Joe Gomez, 27, ananyatiwa na klabu ya Bayern Munich ya Bundesliga. (Mirror)
Chelsea wanafikiria kumpa mkataba mpya kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, ambaye anawaniwa na klabu za Aston Villa na Tottenham. (Guardian)
AC Milan wamefanya mazungumzo na Aston Villa kuhusu mpango wa kumnunua beki wa Poland Matty Cash, 26. (Talksport)
Kocha wa zamani wa Lille na Roma Paulo Fonseca anatarajiwa kuteuliwa kuwa mkufunzi mpya wa AC Milan. (Sky Sports)
Wakala wa kiungo wa Aston Villa Douglas Luiz, 26, amekuwa akiwasiliana na mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil akitathmini chaguo lake la majira ya joto. (Sport - kwa Kihispania)
Mlinda mlango wa Liverpool na Brazil Alisson, 31, amekataa nafasi ya kujiunga na klabu ya Saudia ya Al-Nassr. (Football Insider)
Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anatazamiwa kusaini nyongeza ya miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa. (Telegraph - usajili unahitajika)
Kocha wa zamani wa Chelsea Graham Potter na meneja wa sasa wa West Brom Carlos Corberan ndio wanaoongoza mbio za kuinoa Leicester City. (Athletic - usajili inahitajika)
Chelsea wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth na England Dominic Solanke, 26, msimu huu. (HITC)
Liverpool wanatarajiwa kutoa ofa kwa kiungo wa kati wa Ureno na Benfica Joao Neves mwenye umri wa miaka 19 siku chache zijazo. (Correio da Manha - kwa Kireno)
West Ham wanavutiwa na Max Kilman wa Wolves, 27, lakini beki huyo wa Uingereza anaweza kugharimu pauni milioni 45. (Mail)
The Hammers pia wanavutiwa na mshambuliaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 21, Matias Soule katika klabu ya Juventus. (Fabrizio Romano)
Aston Villa wameanza mazungumzo na Marseille kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 25. (Football Insider)
Fulham wameelekeza darubini yao kwa mlinzi wa Luton Muingereza Teden Mengi, 22, na wanapanga kuwasajili mabeki wawili msimu huu. (Standard)
Beki wa Tottenham Muingereza Djed Spence, 23, amepiga hatua katika mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Serie A Genoa kwa mkataba wa mkopo. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi