Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii 08.09.2022

Fabrizio Romano

Chanzo cha picha, Twitter/Fabrizio Romano

Iliyochapishwa

Ni rasmi, imethibitishwa. Graham Potter ameteuliwa kuwa meneja mpya wa Chelsea. Klabu ya Soka ya Chelsea imemkaribisha Graham Potter kama Kocha Mkuu mpya, akijiunga kwa kandarasi ya miaka mitano katika kuinoa Klabu Hiyo.

Potter ameachana na klabu ya Brighton ya Ligi Kuu ya Uingereza na kuchukua nafasi hiyo na amesaini mkataba wa miaka mitano na The Blues.

Anasema kuwa "anajivunia sana na anafuraha kuiwakilisha Chelsea".

Mchezo wa kwanza wa Potter utakuwa ugenini dhidi ya klabu ya Fulham ya magharibi mwa London siku ya Jumamosi

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Vipimo vya afya vya Diego Costa vimekamilika, kinachosubiliwa ni makubaliano ya mwisho pamoja na vibali vya kufanyia kazi nchini Uingereza kisha atasaini kama mchezaji mpya wa Wolves kwa mkataba hadi Juni 2023, ambao pia huenda ukawa na kipengele cha kuongeza muda lakini bado ipo katika majadiliano.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Nathan Redmond ameaga kwa hisia kali katika klabu ya Southampton baada ya kusajiliwa na klabu ya Besiktas ya Uturuki.

Alichapisha video kwenye Instagram akaishukuru klabu hiyo kwa miaka yake sita aliyoichezea.

Mshambuliaji huyo wa Uingereza ameondoka Southampton na kujiunga na Besiktas ya Uturuki katika uhamisho wa kudumu.

Amekuwa Southampton tangu ajiunge nao kutoka Norwich City mwaka 2016 na alikuwa katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake huko St Mary's.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle wako katika mazungumzo ya mwisho ya kumsajili mlinda mlango wa zamani wa Liverpool Loris Karius kufuatia kuumia kwa Karl Darlow kwenye mazoezi jana.

ggg

Chanzo cha picha, EPA

Mkuu wa Inter Milan anadokeza kwamba mustakabali wa uhamisho wa Romelu Lukaku anaweza kurejea Chelsea baada ya Thomas Tuchel kutimuliwa.

Giuseppe Marotta amesema mazungumzo na Chelsea kuhusu mustakabali wa Romelu Lukaku yataendelea mwishoni mwa msimu huu.

Lukaku alirejea Inter kwa mkopo msimu wa joto baada ya kampeni mbaya huko Stamford Bridge.