Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 26.08.2023

Chanzo cha picha, PA Media
Arsenal wako tayari kuwauza wachezaji tisa ili kupata pauni milioni 100 ili kusawazisha vitabu kabla ya dirisha la usajili kufungwa tarehe 1 Septemba. (Mirror)
Kipa wa Fenerbahce na Uturuki Altay Bayindir, 25, anasafiri kuelekea Uingereza huku akikaribia uhamisho wa £6m kujiunga na Manchester United. (Talk Sport)
Manchester United wamemuweka mchezaji huru Mwingereza Ryan Bertrand, 34, kwenye orodha yao ya walioteuliwa huku wakitafuta mlinzi mmoja kujaza pengo la muingereza Luke Shaw, 28, aliyejeruhiwa. (Express)
Paris St-Germain wanataka kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 21, kwa Brentford, lakini klabu hiyo ya Ligi ya Premia inalenga kujaribu kumsajili winga wa Argentina Nicolas Gonzalez, 25, kutoka Fiorentina. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton wanakaribia kukubali dili la pauni milioni 25.7 kumsaini mshambuliaji wa Udinese Mreno Beto, 25. (Tuttomercatoweb - in Italian).
Mshambulizi wa Lyon Mfaransa Bradley Barcola, 20, yuko tayari kutengua nia ya Chelsea huku akipendelea kuhamia Paris St-Germain. (90 min)
Crystal Palace itadai pauni milioni 70 kwa winga wa Uingereza Eberechi Eze, 25, na kiungo wa kati wa Mali Cheick Doucoure, 23, msimu huu. (Evening Standard)
Liverpool wanatafuta kupata huduma za beki wa Bayer Leverkusen wa Ecuador Piero Hincapie, 21. (four four two)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Corinthians Mbrazil Murillo, 21, yuko mbioni kujiunga na Nottingham Forest. (Fabrizio Romano)
Crystal Palace wamefanya mawasiliano na Paris St-Germain kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Julian Draxler, 29. (RMC Sport - in French)
Nottingham Forest wanavutiwa na Trevoh Chalobah, 24, lakini mlinzi wa Chelsea na Muingereza hana nia ya kutaka kuhamia City Ground. (Football Insider)












