Tetesi za soka Ijumaa: Jaribio la Napoli kumsajili Garnacho lagonga mwamba

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United imekataa ombi la klabu ya Napoli ya Italia la kumsajili winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20 kwa kima cha pauni milioni 40 . (Mirror)
Everton wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Brazil Willian, 36, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Olympiakos mwezi Desemba. (Telegraph)
Manchester City italazimika kulipa pauni milioni 67 kumsajili beki wa Juventus na Italia Andrea Cambiaso, 24, katika uhamisho wa wachezaji wa Januari. (Gianluca di Marzio)

Chanzo cha picha, Getty Images
Borussia Dortmund wameungana na AC Milan kutaka mbio za kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 27. (Florian Plettenberg, Sky Germany)
Arsenal wamekubali masharti binafsi na nyongeza kubwa ya mshahara na kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 25. (Football Transfers)
West Ham na Tottenham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Uhispania Ansu Fati, 22. (Sport )

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wana nia ya kumsajili mlinzi wa kati wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 23, msimu wa joto. (Foot Mercato)
Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imerejelea tena mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah. (L'Equipe)
West Ham wana uwezekfikiria kumsajili mshambuliaji wa Nottingham Forest na Nigeria Taiwo Awoniyi, 27. (Florian Plettenberg)

Chanzo cha picha, Getty Images
Forest itamlenga mshambuliaji wa Brentford na DR Congo Yoane Wissa iwapo Awoniyi ataondoka katika klabu hiyo mwezi huu. (Telegraph)
Dortmund wanavutiwa na winga wa Brentford na Ujerumani Kevin Schade, 23. (Bild)
Atlanta United wametoa ofa ya £15m kwa mshambuliaji wa Crystal Palace Mfaransa Odsonne Edouard, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Leicester City. (Mail)
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Ambia Hirsi












