Jinsi Israel inavyowazuilia mamia ya Wapalestina bila kuwafungulia mashtaka

Iliyochapishwa

Yazen Alhasnat alikuwa ameketi karibu na mama yake mzazi akijaribu kukabiliana na usingizi uliombana machoni katika nyumba hii mjini Bethlehem, iliyopo kwenye Ukingo wa Mgharibi.

Kijana huyu mwenye umri wa miaka 17, alikuwa ameachiliwa huru usiku wa kuamkia siku hii, takriban miezi mitano baada ya kukamatwa katika uvamizi uliofanyika na jeshi la Israel nyumabni mwao , usiku wa manane.

Yazen alikuwa amezuiliwa chini ya mpango wa ‘kizuizi cha mamlaka’ – sera ya usalama ambayo imekuwepo kwa muda mrefu sana, ambayo Isreal ilirithi kutoka kwa uongozi wa Uinregeza. Sera hiyo inaikubalia Israel kuwazuilia watu kwa wakati usiojulikana bila ya kufunguliwa mashstaka mahakamani, na bila ya kuwasilisha Ushahidi dhidi yao. ‘Wana faili ya siri,’Alisema Yazen. ‘Hawakuelelzi kilichonakiliwa ndani yake.’

Alikuwa amerejea nyumbani kwa kuwa alikuwa miongoni mwa watoto na wanawake 180 wa Kipalestina ambao waliachiliwa kutoka kwa magereza ya Israel katika mpango wa hivi maajuzi wa kubalishana wafungwa wa Palestina na mateka kutoka Israel waliozuiliwa Gaza na kundi la Hamas.

Lakini kwa wakati huo huo, wapalestina walipokuwa wakiachiliwa kutoka kwenye magereza ya Israel, Israel yenyewe ilikuwa inazuilia idadi kubwa ya watu katika miaka ya hivi maajuzi. Katika wiki zilizofuatia shambulizi lililotekelezwa na kundi la Hamas Oktoba 7 2023, idadi ya watu ambao walikuwa wanazuiliwa chini ya mpango wa ,’kizuizi cha mamlaka’ – ambayo ilikuwa ya juu zaidi katika muda wa miaka 30 ikiwa na watu 1300 , idadi iliyopanda hadi watu 2800.

Wakati ambapo Yazen aliwachiliwa huru, familia yake ilimarishwa kutosherehekea hatua hiyo hadharani wala kuzungumza na vyombo vya Habari. Maelezo kama hayo, yalitolewa kwa familia nyingine za vijana wawili ambao walizungumza na BBC kuhusu waliyoyapitia kizuizini. Lakini familia zote tatu, zilisema kwamba zililkuwa zimetaka tu kuangazia kuhusu suala la ‘kizuizi cha mamlaka.’

Israel inasema kwamba inatumia mpango huo, ambao unafuata misingi ya sheria za kimataifa n ani mbinu muhimu ya kukabiliana na kudhibiti ugaidi.

Maurice Hirsch, ambaye alikuwa mkurugenzi wa operesheni za kijeshi katika ukingo wa magharibi kati ya 2013 na 2016, ameiambia BBC kwamba Israel haikuwa tu inafuata na kutimiza sheria za kimataifa bali ilipitisha viwango vinavyohitajika’ , kwa kuwakubalia wanaozuiliwa kukata rufaa dhidi ya kifungo chao na kuhakikisha kwamba kuzuiliwa kwao kunaweza kuangaziwa upya kila baada ya miezi sita.

Lakini makundi ya kutetea haki za kibinadamu zinasema kwamba Hatua ya Israel kupanua misingi ya sera hiyo, ni ukiukaji wa sheria za usalama ambazo hazikubuniwa kutumika inavyofanyika na kwa viwango ambavyo wanaozuiliwa hawana uwezo wa kujitetea vyema, kukata rufaa, kwa sababu hawana njia ya kupata ushahidi uliowekwa dhidi yao.

‘Chini ya sheria za kimataifa, ‘kizuizi cha mamlaka,’ inapaswa kuwa njia nadra inayotumika katika hali ya dharura,’ alisema Jessica Montell ambaye ni kurugenzi mkuu wa HaMoked, ambalo ni shirika la kutetea haki za kibinadamu kutok Israel ambalo linachunguza na kuangazia hatua za kuwazuilia Wapalestina.

‘Unapaswa kuitumia sheria hii pale ambapo hatari inajitokea na hamna njia nyingine ya kuzuia harati hiyo ila tu kwa kumzuilia mshukiwa. Lakini, ni wazi kwamba, Israel haitumii sheria hii katika njia hiyo. Inawazuilia mamia, na malefu ya watu bila kuwafungulia mashtaka, na kutumia ,’kizuizi cha mamlaka’ kama kinga yake dhidi ya kuchunguzwa,’

Wapalestina wamakabiliwa na sheria hii ya kuzuiliwa ya ,’kizuizi cha mamlaka’ katika eneo hili tangu 1945, mwanzo chini ya mamlaka ya Uingereza na kisha katika mamlaka iliyosimamia na kuzingirwa ya Palestina.

Sheria hiyo, katika nafasi nadra, imatumika dhidi ya walowezi wa Kiisraeli, lakini inatumika kwa zaidi dhidi ya wapalestina katika Ukingo wa magharibi, wakiwemo Watoto. Wazuiliwa chini ya sheria hiyo ya ,’kizuizi cha mamlaka,’ wanapokea nafasi ya kujitetea – katika mahakama ya kijeshi, mbele ya Jaji au hakimu kutoka jeshi la Israel- ila, serikali ya taifa hilo haihitajiki kuwasilisha Ushahidi wowote uliokusanywa dhidi ya wanaozuiliwa kwa mawakili wao.

Wanaozuiliwa wanawaze kupata adhabu ya kifungo cha miezi sita gerezani. Lakini muda huu unaweza kuongezwa na mahakama hiyo ya kijeshi kwa miezi mingine sita au muda usioljulikana , hali ambayo wengi wanalalmika kwamba wanaozuiliwa mara nyingi hawana ufahamu ni muda gani watasalia gerezani.

‘Kinachokuathiri zaidi akilini ni hali ya kutojuwa kitakachokupata, ‘ alisema Yazen, akiwa amekaa barazani, nyumbani kwao. ‘Je, utakamilisha miezi sita na kuachiliwa huru? Au utaongezewa muda kwa mwaka mmoja, au miwili?’

Wanaozuiliwa wanaweza kuwailisha kesi ya kukata rufaa, hadi katika Mahakama ya Juu zaidi nchini Israel, lakini hali hii hutatizwa na wao kukosa Ushahidi ambao serikali ya nchi hiyo imepata kuwahusu na kutumika kuwazuilia. Kwa hilo, hawana la msingi la kuwasilisha kesi ya kujiokoa. Wapalestina ambao hushtakiwa katika mahakama za kijeshi nchini Israel, wana nafasi bora ya kupata Ushahidi dhidi yao, ila serikali ya taifa hilo inajisifia kwamba ina uwezo wa kushinda asilimia 99 ya kesi hizo.

‘Kwa wakili, jukumu la kuwatetea waPalestina katika mahakama hizo za kijeshi, ni kibarua kigumu,’alisema Maher Hanna, wakili ambaye anafanya kazi Jerusalem.

‘Jinsi mmpangilio ulivyo, ni nadra sana kwa Walapestina kupata nafasi njema ya kujiteta. Ina vikwazo na vizuizi kwa upande wa utetezi na kumuondolea uzito wakili wa upande wa mashataka dhidi ya kuonyesha kwa uhakika aliyekamatwa ana makosa,’

Matumizi ya sheria hiyo ya Israel katika ukingo wa magharibi , ‘ni hatua iliyovuka mipaka ya rangi – nyekundu, kijani na rangi za kila aina,’ alisema mamake Yazen, Saidah.

‘Tunaishi chini ya aina sambamba ya sheria za haki,’

Wakati ambapo Osama Marmesh, kijana mwenye umri wa miaka 17 alipokamatwa, aliondolewa nyumbani na kubwagwa kwenye gari ambalo halikuwa na nambari za usajili, alitueleza. Kwa saa arobaini na nane baada yah apo, babake Naif hakuwa ana fahamu ni wapi haswa alipokuwa akizuiliwa . ‘Unaweza kuwapigia simu wote unaowafahamu kuwauliza ikiwa wanafahamu anapozuiliwa mwanao, ‘ alisema Naif. ‘ Usingizi unakukwepa,’

Osama aliwauuliza mara kadhaa waliomzuilia kuhusu mashtaka yaliyomkabili, alisema, likini kila mara alipofanya hivyo alipokea jibu la, ‘nyamaza kimya,’

Alipokamatwa Musa loridat, mwenye umri wa miaka 17, katika uvamizi was aa kumi na moja alfajiri, nyumbani mwao, wanajeshi wa Israel walisaka chumba chake cha kulala ambacho wanalala ndani na kaka zake wawili wadogo. Walipovuruga vitu wakitafuta ambacho hawakukitaja, walifyatua risasi kwenye kabati, na kuvunja glasi za madirisha ,’ alisema.

‘Alipokamatwa, aliondoshwa akiwa tu amevalia nguo ya ndani, alisema Mohammad ambaye ni babake Musa, huku akituonyesha picha ya yaliyojiri kwenye simu yake. ‘Kwa siku tatu, hatukuwa tuna jua lolote,’

Yazen, Osama, Musa, wazazi na mawakili wao hawakuonyeshwa Ushahidi uliokusanywa dhidi yao katika miezi ambayo walikuwa wanazuiliwa gerezani. Wakati ambapo Israel ilichapisha orodha ya wafungwa ambao walitarajiwa kuachiliwa huru, katika mpangon wa kubalishana wafungwa na mateka, katika nafasi ya kunakili mashtaka waliokabiliwa nayo watatu hao waliandikiwa kwamba ‘ wao ni tishio kwa usalama wa eneo hilo,’

Katika orodha nyingine ambayo ilitolewa Yazen na Musa waliandikiwa mashtaka ya kushukiwa kuwa na uhusiano na makundi ya kivita ya kipalestina. Osama alipoachiliwa huru, aliandikiwa shtaka la kwamba katika siku mbili ya miezi ya awali, aliwahi kurusha mawe yenye kutoshana na mkono wake kwa upande wa wamajeshi wa Israel,’

Maurice Hirsch, ambaye alikuwa mkurugezi wa zamani wa mashataka katika mahakama ya kijeshi, amesema kwamba itakuwa makosa kufanya mamauzi kutokana na taarifa chache ambazo zimetolewa. ‘Kuna tofauti kubwa sana kati ya Ushahidi ulio wazi dhidi ya magaidi hawa watatu na taarifa za kijasusi ambazo tunazo, alisema. ‘Tunaona sheria hii ya ‘kizuizi cha mamlaka’ ikitumiwa na Wamarekani katika gereza la Guantanamo Bay, kwa hivyo tunajuwa kwamba hatua hii inatambulika kimataifa na kukubalika kama mbinu mwafaka,’ aliongezea. ‘ na kwa sababu ni sheria ambayo inatambulika kimataifa , ni kwa nini ni Israel tu inazuiliwa kutoitumia, wakati ambapo tunakabiliwa na tishio kubwa zaidi ya ugaidi ambayo haijawahi tena kuonekana?’

Mwishoni, Yazen, Osama na Musa walikuwa gerezani kwa muda kati ya miezi minne na saba. Wote watatu, walisema kwamba hali ndani ya gereza zilikuwa si haba, hadi pale shambulizi la kundi la Hamas lilipotekelezwa Oktoba 7, ambapo shiti za kulalia,blanketi na mavazi ya ziada na vile vile chakula ziliondolewa na mawasiliano yote na walio nje ya gereza ilikatizwa, katika hali ambayo wanaeleza ilikuwa njia ya kuwaadhibi wote kwa yalioyotokea kwenye shambulizi la Hamas.

Wafungwa wengine wamedai kuchapwa, kurushiwa mabomu ya kutoa machozi na hata kuvamwia na mbwa.

Yazen, Osama na Musa waliachiliwa mampema, kwa sababu mpango wa kubalishana wafungwa na mateka uliangazia wanawake na Watoto. Lakini kulingana na takwimu za hivi punde kutoka kwa idara ya magereza, bado kuna watu 2,873 ambao wanazuilia chini ya sheria ya ,’kizuizi cha mamlaka’ katika magereza ya Israel.

Siku moja baada ya kurejea nyumbani, Musa alikuwa chumbani mwake, alipokamatwa kutoka kwa kitanda chake na kulazimishwa kuingia kizuizini na wanajeshi wa Israel, miezi minne iliyopita.

Milango ya kabati, iliyoharibiwa na risasi, ilikuwa imeondolewa, ili kutengezwa, lakini chumba kilikuwa kimetengezwa na wazazi wake. Musa alikuwa amejiandaa kuwa gerezani kwa muda mrefu alisema. Wakili wake alimueleza kwamba kulikuwa na uwezo mkubwa zaidi kwamba kifungo chake kingeongezwa muda.

Wavulana wote watatu, wamesema kwamba, watajaribu kukamilisha masomo yao shuleni licha ya maisha wanayokumbana nayo ya kukabiliana na tisho la kukamatwa na kuzuiliwa tena, wanasema ni hali ambayo inawapa msongo wa mawazo unaowafunga akilini, alisema Musa.

‘Walituachiliwa huru na kutukabidhi kwenye gereza kuu la Maisha,’ alisema Yazen.

'‘Hamna amani,’ alisema mamake Yazen, akimtazama mwanawe. ‘Wanaweza kukumata, wakati wowote.’'

Idara ya magereza ya Israel, imethibitisha kwamba iliweka magereza yake katika hali ya hatari na kupunguza huduma muhimu kwa wafungwa kwa misingi ya kiusalama katika operesheni iliyofuatia shambulizi la kundi la Hamas.

Imetafsiriwa na Laillah Mohammed